kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Mkurugenzi wa kampuni ya Principal Company Limited, Godfrey Mosha ambaye ni mmoja wa washitakiwa wa kesi ya wizi wa pesa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ameieleza mahakama jinsi Benki ya Akiba Commercial (ACB), tawi la Kariakoo ilivyoidhinisha malipo ya pesa kwa mtu mwingine kutoka kwenye akaunti yake.
Mbali na Mosha washitakiwa wengine ni Bahati Mahenge, Manase Makale, Davis Kamungu na Eda Makale, wanakabiliwa na kesi ya wizi wa Sh. bilioni 1.86 za EPA katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wanadaiwa kuiba fedha hizo kuipitia kampuni ya Changanyikeni Residential Complex.
Mosha alitoa ushahidi huo mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu Warialwande Lema na kudai kuwa benki hiyo ilitoa Sh. milioni 46.8, zilizolipwa kwa mtu aliyetambulika kwa jina la Rafael John kwa kutumia hundi nne tofauti na tarehe tofauti.
Alidai kuwa benki hiyo ilimpa fedha mtu asiyemfahamika na alibaini kuwa hamisho hilo katika akaunti yake namba 0400438671lilifanyika Novemba 15, 2011, baada ya kuchukuwa taarifa ya benki.
Alidai baada ya kubaini hamisho hilo la pesa, alikwenda makao makuu ya benki hiyo na alimuona Meneja wa Fedha, Vincent Antony na kumweleza kuhusu tukio hilo.
Alidai kuwa baada ya kuonana na Vincent alimuambia kuwa siyo hamisho bali ni malipo yaliyofanyika kwa kutumia hundi na kumwambia namba za hundi hizo na ilionekana kuwa zililipwa kwa Rafael John Mkwabi, mwenye akaunti namba 11000787541.
"Huyo John mi sijawahi kumwandikia hundi, wala sijawahi kufanya naye biashara, sijawahi kukutanana naye wala simfahamu," Mosha alidai na kuongeza kuwa hundi hizo zilikuwa zimesainiwa na Vicent na Meneja Mkuu, Salehe Ramadhani, huku akidai kuwa saini inayoonekana katika hundi hizo si yake na kutaja hundi hizo kuwa ni namba 083722, ya Sh. milioni 11.6 iliyolipwa Novemba 11, 2011 na namba 083723 ya Sh. milioni 9, pia iliyolipwa tarehe hiyo.
Hundi nyingine ni hundi namba 083724 ya Sh. milioni 14.4 iliyolipwa Desemba 2011 na namba 083725 ya Sh. milioni 11.8 iliyolipwa Desemba 3, 2011.
Moshi aliziwasilisha hundi hizo pamoja na nyaraka mbalimbali zinazoonyesha saini yake halisi mahakamani hapo kama vielelezo vya ushahidi katika kesi hiyo.
Hata hivyo, Hakimu Lema aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 8, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
CHANZO: NIPASHE