mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Arusha.
Mshitakiwa wa tatu katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, Daniel Laurent Mbura (31), ameieleza mahakama kuwa hamtambui mshitakiwa wa kwanza wala wa pili katika shauri hilo na alifahamiana nao walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 4.
Akijitetea mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo shahidi huyo pia amekanusha majina yaliyopo kwenye hati ya mashitaka ambayo yanasomeka kama Daniel Gabriel Mbura wakati yeye jina lake ni Daniel Laurent Mbura.
Shahidi huyo aliiomba mahakama kupokea vyeti vyake viwili kuthibitisha majina yake na mahakama ikavipokea.
Akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili anayemtetea, Fridolin Gwemelo, mshitakiwa wa tatu katika shauri hilo alisema Februari 9 alikuwa nyumbani na hakutoka siku nzima.
Chanzo;Mwananchi