Mshtuko kabla ya kulala

blackberry m

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
563
Reaction score
414
Habari za jioni wakuu…

Poleni na majukumu ya kulijenga taifa na kujitafutia chochote kile ili mkono uende kinywani.

Nia na dhumuni langu kuandika waraka huu, ni kupata usaidizi/ushauri na hata utatuzi/tiba ya tatizo linalonisumbua. Tatizo langu naweza kuliita la pekee (najua ninalo peke yangu), kwani sijawahi sikia au soma mtu akiwa ameandika humu ukiachilia mbali kusimulia.

Tatizo ni kwamba, kabla ya kulala au kuchukuliwa na usingizi ni lazima nipate mshtuko kidogo ndipo niweze kulala. Ni muda sasa kwani nakumbuka kuwa nilikuwa nalo tangia zama zangu za utoto hata sasa.

Nakumbuka nyakati za utoto nilikuwa nahisi kama naruka kwenye mti (kudondoka), kisha nikishtuka na kulala tena hiyo njozi haijirudii tena hadi ifike siku nyingine.

Sasa nyakati hizi njozi hizo hakuna ila najikuta nashtuka tu na kisha kufuatiwa na usingizi mzito. Yeyote mwenye kufahamu na kujua tiba rasmi ya tatizo langu, tafadhali asisite kunieleza.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu…
 
mkuu hilo tatizohata me ninalo na limeacha sasa hivi lakini nilikua sipitiwi na usingizi mpaka nishtuke na sjui inasababishwa na nn kwa kweli
 
Ngoja tusubiri wataalam waje
tena wakat mwengine nakua nishapitiwa na usingizi inanijia njozi naota napanda ngazi halaf mara ghafla kufika ya juu kama nimejikwaa mshtuko wake hapo naweza ruka hata kitandani halaf ndio nalala kwa amani kabisa ngoja tusubirie mkuu
 
 
Ni tabia ya mwili kujilinda na shambulio lolote lile ili kuhakikisha kuwa unaendelea kuishi,hutokea ili kuuweka mwili wako katika hali ya kawaida ikiwemo kupumua sawasawa(mapafu yanahusika) na kuhakikisha damu inazunguka sawasawa(Moyo unahusika) ili viendelee na kazi kama inavyopasa kuwa.
 
Nimekuelewa mkuu. Kwa haya maelezo sitakuwa na shaka tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…