Mshukiwa wa dawa za kulevya aliyetajwa na Mwakyembe!

Mdakuzi

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
4,294
Reaction score
6,872
Waziri wa uchukuzi Prof. Harrison Mwakyembe amemtaja mshukiwa mmoja wa dawa za kulevya aitaye Nassoro Mangunga, lakini mshukiwa huyu pamoja na picha zake alishaandikwa na gazeti la SANI katika toleo lake la Agosti 7-9, 2013 (toleo la 1042) pamoja na namna alivyosafirisha mzigo pamoja na akina Masogange.

Isome taarifa yao:


Na Mwandishi Wetu
Unaweza kukimbia lakini huwezi kujificha. Msemo huu unaonekana kutimia kwa kijana anayedaiwa kuambatana na watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa Julai 5 mwaka huu nchini Afrika Kusini, Agness Gerald 'Masogange' (25) na Melisa Edward (24), kunaswa na gazeti hili.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, wasichana hao, Masogange na Melisa walisafiri ndege moja na kijana anayejulikana kwa jina la Nassoro Mangunga wakitoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini, wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), yenye namba SA 189.
Wakiwa katika ndege hiyo Mangunga, Agness na Melisa walikaa kwenye viti vilivyo jirani kabisa huku Mangunga akiwa katikati yao, kwani Agness alikaa kiti namba 23B, Mangunga alikaa kiti namba 23D na Melisa alikaa kiti namba 23A.
Mangunga ambaye ni rafiki mkubwa wa wanamuziki wa Bongo Flava, Rashidi Abdallah Makwiro 'Chid Benz', Mgaza Pembe 'M2theP' na Albert Keneth Mangweha 'Mangwair', wakati akisafiri na mabinti hao walikuwa na jumla ya mabegi tisa kama kumbukumbu za nyaraka za shirika hilo la ndege zinavyoainisha.
Licha ya nyaraka za kusafirishia mabegi hayo kuonesha jina la Agness Gerald ambaye ni mpenzi wa Mangunga tangu mwanzoni mwa mwaka jana, kuwa ndiye aliyelipia mabegi hayo, ila kwenye sehemu ya anuani ya waraka pepe, imeandikwa ya Mangunga (inahifadhiwa) ya tovuti ya Gmail.
Aidha, mabegi hayo, yalikuwa na kilo 150 za dawa za kulevya lakini kila mmoja alitakiwa kusafiri na kifurushi cha kilo ishirini kama mzigo wa mkononi ambao husafiri bila malipo, hivyo watatu hao kwa pamoja walikuwa na kilo sitini wote kwa pamoja, hivyi kubaki kilo 90 ambazo walizozilipia Dola za Marekani 94 badala ya Dola 450.
Mangunga ambaye licha ya kuishi zaidi nchini Afrika Kusini, lakini pia ni mkazi wa maeneo ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Agness na Melisa, walikamatwa Julai 5, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo, Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8 za Kitanzania, na walipotiwa mbaroni, walikuwa na mabegi sita tu kati ya tisa waliyokuwa nayo wakati wanapanda ndege jijini Dar es Salaam.
Inasemekana mabegi hayo matatu yaliondoka na Mangunga na kutokomea kusikojulikana, jambo linalolifanya Sani kuzamia zaidi ili kuweka mezani timu nzima inayohusika na mzigo huo.


Mangunga mwenyewe
 
Duu mzee kweli kajitoa muhanga hope zaidi ya huyo atatangazwa pia
 
mjini hapa watu wanaendesha magari mazuri...wanachezea hela...unashangaa watu wanapata wapi kumbe ...dah
 
Dr.Mo umeandika kwa hisia sana hapo juu.ni kweli kabisa ukiwaza sana unaweza kuchanganyikiwa,na hasa hapa dar watu wana mitandao yao na maisha ya anasa sana kwa deal hiii,na hii si biashara hii ni deal tu
 
Last edited by a moderator:
iwekwe sheria ya kuwanyang'anya mali zao zote ikiwamo Nyumba na magari. halafu serikali iwatoze kodi kwa miaka kumi nyuma, kwamba wamefanya biashara bila kulipa kodi. Hilo deni wahakikishe wanalilipa mara watokap[o jela ya miaka 25. hap unga utakoma kuuzwa kama njugu.
 
Dr.Mo umeandika kwa hisia sana hapo juu.ni kweli kabisa ukiwaza sana unaweza kuchanganyikiwa,na hasa hapa dar watu wana mitandao yao na maisha ya anasa sana kwa deal hiii,na hii si biashara hii ni deal tu
Mkuu mkorosho kigoli.....watu wanakula bata siku nzima na hela wanayo mingi.....mpaka unajiuliza hizo ramani zao kachora nani....a/ kumbe dah....mcheki mwakyembe utajua watu wanavyopiga deal kijinga...
 
Police wanafanya nini mpaka mtu kama Waziri awatangaze wauza unga? Hivi vyombo vya ulinzi hamuoni aibu? Ninyi Polisi na Usalama wa Taifa mko mko tu? Ninyi TAKUKURU mnafanya nini? Watu wa Uhamiaji? Bandari na viwanja vya ndege... are you serious na hatma ya nchi? Shame on you....
 

Kufilisiwa naunga mkono. Ila wakishafilisiwa wafungwe jela maisha, tena kifungo cha maisha na kazi ngumu, wasipewe nafasi kama zile za VIP Papaa Msofe. Ati mtu yuko ndani anatembelewa na jamaa zake, anafanya biashara zake akiwa jela! Haiyumkini uhayawani kama huu ukaruhusiwa kuendelea! Wafungwe maisha kabisa, wasipewe msama wa rais na wasipewe parole! Iwe fundisho!
 
Hapa ishu ya mwakyembe kuingilia swala la madawa ni strategy ya kuwapumbaza watu na kutufanya tuone tunafika kwenye suluhisho la hili tatizo. Na kwa reputation yake wengi wanaamin anapambana kweli bt kiukwel kawekewa limit ya ku deal na hii ishu.
Tunaweza kujiuliza mamlaka ya kuwafukuza askari kaitoa wap?au kuwabadilishia post tu hao walinzi wa airpot anaweza vip? Hajaagizwa kwel?

kingine habari inadai kina masogange walikuwa na mabegi 9, well but airpot SA walikamatwa na begi 6 so 3 hazikukamatwa! Packaging ni kwamba walikuwa na kilo 60 za madawa kama mzgo wa mkononi kwa kila mmoja na kilo 90 kama mzgo wa zaida. So kama walikamatwa na begi 6 manake walikuwa na kilo 60 na hizo beg 3 ndo zilikuwa na hizo kilo 90 kama mzigo wa ziada.

kama huyo mshkaji alikimbia na beg 3 akawatoa mhanga kina masogange ili atembee na huo mzigo mwingne of which the plan work as jamaa hakukamatwa na hizo beg 3 hazikuonekana huko SA.

Na huyo mshkaji ndo mwenye huo mzigo au yeye alikuwa ana monitor tu usafirishaji? Manake hilo halijawekwa waz na mh. Wazir.
 

...kwenye nyekundu, "ukiwa na urafiki na mwizi, lazima na wewe utakuwa mwizi"

'wote watajwao hapo juu wakamate ili kusaidia upelelezi'
 
hii kitu nillikuwaga najiuliza sana hivi mimi nina nini naona vijana wa umri kama wangu wanasukuma mikoko ya bei mbaya mimi nagombea daladala kila siku kila nikijitahidi kufanya kazi kwa bidii na kujibana sana bado nakuwa napiga hatua kwa tabu sana lakini vijana wenzangu kila kukicha na mikoko mipya kumbe ndivyo walivyo
 

I second you!
 
Oikos, Polisi wetu na vyombo vyetu vya usalama wako bize kupambana na Wapinzani wa CCM tu, mlango wa nyuma wanashiriki kwenye ufisadi kama huu, na kwa kuwa wanawafurahisha watawala kwa kuwaminya wapinzani, CCM na serikali yake wanajifanya hawaoni wala kujua kinachoendelea.

Usishangae kusikia Rais na PM wakijikausha na kujifanya hawaoni wala kujua jitihada za Dr Mwakyembe kuwawajibisha wafanyakazi wa JNIA.
 
Sasa wanahangaika nini kwani hakuna Interpol? Waweke wanted tu kama alivyodakwa Alex massawe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…