Mshukiwa wa mauaji Kevin Kang'ethe arejeshwa Marekani kujibu mashtaka

Mshukiwa wa mauaji Kevin Kang'ethe arejeshwa Marekani kujibu mashtaka

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
1725284959623.png
Mshukiwa wa mauaji Kevin Kang'ethe amesafirishwa kutoka Kenya hadi Marekani kujibu mashtaka ya kumuua mpenzi wake Margaret Mbitu.

Kupitia idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga, Kang'ethe alifaulu kurejeshwa Jumapili na atakabiliwa na kesi mjini Boston Jumanne, Septemba 3.

Katika taarifa yake kwa vyomba vya habari, DPP Ingonga alithibitisha dhamira yake ya kuunga mkono Marekani, hasa timu ya waendesha mashtaka wanapoendelea na awamu inayofuata ya kesi hiyo.

Hapo awali Ingonga alikuwa amemhakikishia Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray mnamo Juni 2024 kwamba ofisi yake ina nia ya kuhakikisha haki inatendeka.

1725284802287.png
Kang'ethe anasakwa nchini Marekani kwa mauaji ya Mbitu, mwenye umri wa miaka 31 ambaye mwili wake uligunduliwa ndani ya gari katika uwanja wa ndege wa Boston Logan mnamo Novemba 2023. Mwathiriwa aliripotiwa kuwa mpenzi wake.

Kisha mshukiwa alikimbilia Kenya na kujificha hadi alipokamatwa na mamlaka ya Kenya.
Baada ya kukamatwa mwezi Januari na kupewa agizo la kuzuiliwa kwa siku 30 ili kuruhusu mamlaka kufanya uchunguzi zaidi, Kang'ethe alitoroka kwa njia ya kutatanishakutoka kwa Kituo cha Polisi cha Muthaiga.

BBC Swahili
 
CHAPUTA na KATAA NDOA walikuwa sahihi kabisa kwenye maamuzi yao.
 
Miaka 31 mtu anakudhurumu uhai kisa mapenzi.
She was so beautiful maskiini, pengine ndiyo tegemeo pekee kwa familia, with a lot to accomplish for her bright future, binadamu ni wakatili mno..!!🙌
 
Back
Top Bottom