SoC02 Mshukuru Mungu kwa hili, soma hii tafadhali...

SoC02 Mshukuru Mungu kwa hili, soma hii tafadhali...

Stories of Change - 2022 Competition

Amani Dimile

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
243
Reaction score
399
Sifa zilizokupatia kazi, ndio sifa hizo hizo mtu fulani anazo lakini hana kazi. ๐— ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Maombi ambayo Mwenyezi Mungu amekujibu, ndio maombi hayo hayo wengine wanayaomba kila siku lakini hawajibiwi bado. ๐— ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Barabara unayovuka kila siku kwa usalama, ndio bara bara hiyo hiyo wengi wao wamekufa pale. ๐— ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Usingizi unaolala na kuamka salama, ndio usingizi huo huo wengi wao wamelala na kutoamka tena. ๐— ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Mvua iliyonyesha ikastawisha mazao yako, ndio mvua hiyo hiyo iliyoharibu mazao ya mwingine. ๐— ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Jua linalokuchoma na unalalamika linawaka sana, ndio jua hilo hilo mtu tangu azaliwe hajawahi kuliona. ๐— ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Ugonjwa ulioumwa, ukatibiwa ukapona. Ndio ugonjwa huo huo mwingine kaumwa akafa. ๐— ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Chakula unachokula unasaza, ndio chakula hicho hicho mtu fulani anakililia kakikosa. ๐— ๐˜€๐—ต๐˜‚๐—ธ๐˜‚๐—ฟ๐˜‚ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚

Hakika, maisha yetu yapo chini ya anga moja lakini yanatofautiana sana Kwa Kila mtu. Penda kumshukuru sana Muumba wako, mapenzi yake ndio yamekufikisha wewe hapo ulipo wala si kingine.
"๐—”๐—ต๐˜€๐—ฎ๐—ป๐˜๐—ฒ ๐˜€๐—ฎ๐—ป๐—ฎ ๐— ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ด๐˜‚ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐—ฒ๐—ป๐—ด๐—ถ ๐˜‚๐—น๐—ถ๐˜†๐—ผ๐—ป๐—ถ๐˜๐—ฒ๐—ป๐—ฑ๐—ฒ๐—ฎ"

Wako katika kalamu โœ๐Ÿผ
Amani Dimile
 
Upvote 0
Back
Top Bottom