Katika mahojiano yangu na mtangazaji Maureen Minanago wa TBC1 mtayarishaji wa kipindi Kurasa Darasa tukizungumza kuhusu utunzaji wa kumbukumbu nilimwonyesha picha ya Mzee Mshume Kiyate na Julius Nyerere iliyopigwa mwaka wa 1964 baada ya maasi ya Tanganyika Rifles (TR).
Picha hii amenipa Mzee Kissinger.
Katika kipande hiki cha video namweleza Maureen Minanago udugu uliokuwapo kati ya Mshume Kiyate na Nyerere katika miaka ile ya kupigania uhuru wa Tanganyika.