Msiba mkubwa

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
1,222
Reaction score
776
Nimefiwa na Mama Yangu Mzazi Hospitali ya Selian Mjini Arusha.
Alikuwa na tatizo ya maji kwenye mapafu. Nashauri tuwe tunapima afya zetu kwani tatizo kama hili likijulikana mapema linatibika. Kama bado una wazazi wanakutegemea wasaidie kuwacheki afya zao kwani unaweza sogeza umri wao mbele

Sisi lilijulikana late so it was too late.

Asanteni sana.
 
Pole sana mkuu, Mwenyezi Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu. RIP Mama BB
 
Pole sana ndugu yangu, Na nashukuru kwa ujasiri wako wa kuikumbuka JF hata kwa wakati mgumu ulionao. Ni upendo wa kweli umeonyesha kwetu. Mungu amlaze mahali pema.

HP
 
Pole sana kamanda....roho ya mama ipumzike mahali pema peponi......
 

Blue Balaa pole sana msiba upo wapi na mazishi yatafanyika wapi?
 
pole sana mkuu! NAKUTAKIA MOYO MKUU!
 
Pole sana BB kwa msiba mzito, Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu. asante pia kwa ushauri wako.
 
pole sana ndugu yangu! kila nafsi itaonja mauti, kikubwa ni kumwomba Mungu atunusuru na maovu ya dunia hii.
 
pole sana ndugu yangu! kila nafsi itaonja mauti, kikubwa ni kumwomba Mungu atunusuru na maovu ya dunia hii.

Pole sana mkuu..msiba wa mama unauma sana...tukuombee tuu mungu akupe ujasiri katika kipindi hiki kigumu kupita vipindi vyote duniani...sisi sote tu njia moja ni wakati sasa umefika tuamini kuwa kifo kipo na tunapita wote...RIP Mama
 
pole sana mkuu. uchungu wa kufiwa na mzazi hausemeki, mm pia yalishanikuta,
JIFARIJI NA UJIPE MOYO MKUU UKIJUA KWAMBA, kWA MUNGU TUMETOKA NA HUKO HUKO TUTAREJEA.
WAKRISTO TUNAAMINI KUISHI NI KRISTO NA KUFA NI FAIDA.
LALA SALAMA MAMA!
 
Asante kwa taarifa.
Na pole sana pia Mungu akupe nguvu katika kindi hiki kigumu.
 

Pole sana kiongozi, mungu akujaalie faraja kwenye kipindi hiki kigumu!
 
Pole sana mkuu
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya mama kwenye mwanga wake wa milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…