Msiba Msibani

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
Msiba msibani

1 Utaona ni rahisi, kama haijakupata
Na vingi utavihisi, hadi utapojipata
Utalia na kamasi, msaada hutapata
Ukiupata msiba, ni msiba msibani

2 Maumivu ni makali, na kufa utatamani
Ima uwe kwa Jalali, au uwe kwa shetani
Hutaona afadhali, dunia iwe chumbani
Ukiupata msiba, ni msiba msibani

3 Hakuna panapo mwanga , kote unaona giza
Watajua umepanga, ufanye unaigiza
Unaweza shika panga, uwende kuyalipiza
Ukiupata msiba, ni msiba msibani

4 Mwishowe unajinyonga, watasema umerogwa
Wanageuka vinyonga, na wakilia na kugwa
Na tena ukijitenga, watasema unanongwa
Ukiupata msiba, ni msiba msibani

5 Unahisi peke yako, shida kawa ndugu yako
Kubeba mzigo wako, katika dunia yako
Yageuka mate yako, machungu kinywani mwako
Ukiupata msiba, ni msiba msibani

Abuuabdillah [emoji3578][emoji1241]
jumaomari@ymail.com
0718569091
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…