Msiba wa King Majuto: Aibu yako Kikwete, aibu yetu Watanzania...

Ki
Kifo hakina huruma ikifika saa ya mja haizuiliki kuna huyu bwana Steve Jobs hakuhitaji msaada wa rais kupata matibabu na alifariki kwa ugonjwa.
 
Mimi Ndio Nashanga "Ameondoka" Uchumi Wake Upo Chin Sanaaa Wkat Kaanza Sanaa Miaka Ming Nyumaa...Au Ndio Namna Kila Mtu Anavyozichanga Karata Zake?
 
Jk nae ni binadamu kama wewe anasahau afu kuna siku alimwambia majuto anaenda kumuombea msaada kwa magu
 
Hakuna lolote.. tumuache mzee wa watu apumzike.

Kwani wasanii si mnapata pesa nyingi tu..? Jijengeeni utaratibu wa kujisevia na kuwekeza..sidhani kama kuna mtu mwenye jukumu la kukununulia au kukupa tu kisicho chako...tuache lawama za kimaskini..
Tena kwenye shughuli zao anamuona mtu anakwenda kutunza mamilioni halafu baadae mtu huyo huyo anaomba pesa za matibabu
 
Ina maana Majuto hakuwa akipata pesa kutokana na kazi zake?
Kapata nyingi sana na kampuni alizofanya nazo kazi zimeorodheshwa hapo juu!

Neel Salt
DSTV (Maisha Magic)
Al Riyami
Super Banco
Airtel
LAPF (staafu kwa ufahari)
ASAS dairies (pipi za Ivori na ivori cocoa powder)
Azam (Maziwa)


...to mention a few.

King Majuto hakuwa mtu wa kuomba msaada wa matibabu iwapo mikataba yote hiyo ingemlipa vizuri. Aliliongelea sana hilo Mhe. Mwakyembe
 
We naye fyatu tu, msanii badala ya kuomba sheria bora za usimamizi wa kazi zao aombe tractor kweli?? Hivi wasanii wote wakiomba matractor nani atatuburudisha?, sema hapa serikali inapaswa kuona aibu mana kwa msanii mkubwa kama yule kufa masikini ni udhaifu wa serikali kutokua na sheria zinazowanufaisha wasanii, mfano jana taifa zaidi ya asilimia 60 watu walivaa bidhaa zenye nembo ya Simba feki, Club haikunufaika na chochote zaidi ya viingilio, ila wote tungekuwa tumenunua bidhaa halisi za Simba team yetu ingefika mbali kiuchumi.

Bado tuna sera mbovu sana, tena mtu anauuza bidhaa (jezi,skafu, culture n,k) feki mbele ya askari na hakamatwi.
 
Ccm haina msaada wowote kwa wasanii zaidi ya kuwatumia kipindi cha kampeni
 
Huyu bibie analalamika kila kitu!
Mwache!
 
Watanzania mna hasira! Hahaha..

Okay nawatoa kwenye lawama, nabakisha ya JK na BASATA..

Kama mngenisoma vizuri, mngeelewa mantiki yangu.

Kikwete hata asingempa trekta, kwa nafasi yake bado alikuwa anao uwezo wa kuagiza mamlaka za chini yake ziangalie namna ya kumnufaisha au kuwanufaisha wasanii na kazi zao..

Hii mikataba mnaitaja taja tu lakini wasanii wanapigwa kinoma na hawana ubavu wa kujitetea. Mamlaka zina nguvu ya kuhakikisha hawaonewi!

Hili ni dongo kwa mamlaka. Msome katika urari huo!
 
Kwetu huwa tunafanya sherehe mzee wa makamo yale kufariki. Maana umri uliobakia ulikua ni umri wa kushambuliwa na magonjwa, hivyo kumfanya ateseke maishani mwake
 
"Kupunguza risk ya kufariki?"

Wakati ukifika umefika ndio naamini hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…