Msiba wa King Majuto: Aibu yako Kikwete, aibu yetu Watanzania...

Hizi ni akili za ombaomba! Tanzania kuna maelfu ya wastaafu wa kila fani. Kwanini unadhani wasanii pekee ndiyo wenye haki ya kusaidiwa? Tena wako wengine wengi ambao kipato chao hakikuwa kikubwa. Jukumu la kuandaa maisha baada ya kustaafu la mtu binafsi na si kutegemea kuomba.
 
Kuna baadhi ya watu nikisoma mawazo yao huwa natamani itungwe sheria ya "mpiga kura lazima awe na kiwango fulani cha IQ"...
Mkuu unajua hata mimi hili swala naliwazaga sana..hii nchi yetu inabidi watu wachache wenye elimu au niseme IQ na exposure fulani ndo wapige kura..maana hii nchi ujinga ndo unaotusumbua
 
Mwishowe Nyie wasanii mtataka mtawazwe pia

Ova
Bwana we... jamaa huwa wanafikiri wana haki ya kusaidiwa wanapougua au kustaafu. Vijijini kuna maelfu ya wakulima ambao wameingiza fedha nyingi za kigeni kwa kuzalisha mazao kama pamba, kahawa na korosho na wanapougua au kustaafu wanajigharamia sembuse hawa wasanii ambao hawaingizi fedha yoyote sana sana wanaendekeza starehe!
 
Me nataka nipate neno moja kutoka kwa mzee wa rambi rambi Tanzania maana hii naona itakuwa dili nono kwake
 
Mimi Ndio Nashanga "Ameondoka" Uchumi Wake Upo Chin Sanaaa Wkat Kaanza Sanaa Miaka Ming Nyumaa...Au Ndio Namna Kila Mtu Anavyozichanga Karata Zake?
Kuna msanii mmoja wa bendi kongwe kwa sasa ni marehemu alilalamika kwamba kazi ya muziki haijamwezesha hata kununua baiskeli na kijana mmoja msanii akamnunulia gari ...wakati huo huo aliwahi kuhojiwa na kusema mwaka 1978 alikuwa anapata 3000 kwa mwezi ambayo ilikuwa hela ya kufanya uendeshe maisha kama wazee wetu walivyojikongoja mpaka leo hii tupo kwenye key board ...lakini mwisho wa siku na sie wananchi tunaingia kwenye mkumbo wakipata matatizo tunalia nao wakati wote ni walala hoi tu
 
Hivi pesa yote aliyokuwa anapata kwenye uigizaji na matangazo alihifadhi wapi mpaka waombe pesa ya kununua tractor ambapo ni kati ya 35 to 50m? Huyu mzee alikuwa sawa na wasanii wengine waliokuwa masikini huku wakati wa uhai wao walikuwa bata tu Hivi kima cha chini cha mshahara aliyajiriwa unaufahamu? Kima cha chini mshahara cha mwalimu unaufahamu? Wengine kwa mwaka mzima hata mshahara wa 4m hapati wakati kazi za sana hata upunjwe vipi hukosi mil 10 kwa mwaka. Yaani hata leo hii ungesema tuchangie mazishi ni udhalilishaji kwa jamii. Pengine ulaumu serikali kwa kuwa na taasisi mbovu za kuratibu wasanii. Ila wenye akili na Mipango mzuri wanatoka vizuri tu. Hivyo asilaumiwe Kikwete wala Serikali ila walaumiwe wasanii wasiokuwa na Mipango madhubuti ya mapato yao.
 
Alikuwa na uwezo sana tu Mzee wetu, alikuwa na HiAce kadhaa, Noah na kajenga na msikiti na madrasa yake nzuri tu. Kwa kauli yake alikuwa anatubu kwa yale alioyafanya wakati wa kazi zake za Sanaa! Mleta mada acha kuwajengea wafiwa chuki na viongozi wao!!!
 
Dah mleta mada sijui kama utakuwa sawa kichwani kwako kwainshu kubwa kama msiba unalinganisha natrekta au ndio msiba umekuchanganya nn
 
Kuna watanzania walikuwa wanatamani nao wapate kazi za matangazo ya biashara alizokuwa anazifanya Mzee Majuto akiwa na Makampuni ya Azam e.t.c lakini hawakuwai kuzipata..Maana yangu ni kwamba kuna watanzania ambao hawajui kama wataweza kumaliza siku hata kwa kupata mlo mmoja wao hawakuwahi kuomba hata jembe kwa JK..iweje yeye na vipaji vyake vyoote achilia mbali pesa alokuwa anaingiza..Muache mzee wa watu apumzike mada nyingine kama mimi ningekuwa 'admin' nazifutilia mbali tena kwa onyo kali...'bullshit' umeandika kaka...
 
Watanzania kwa lawama hamjambo. Mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani
Umeona eh? Sasa kila mtu akimwomba JK trekta, afu akampatia kila mtu inamaana Tanzania hakutakuwa na msiba tena?

Leo ndo nimegundua kumbe trekta ndo kinga ya kifo.

Ngoja niwahi SUMA JKT
 
Ukisikia lawama ndio hizi.
Sasa JK anahusikaje.
Mtu kaanza kuigiza kabla ya JK hajazaliwa. Leo hii lawama kwa JK.
Mpumzisheni JK.
Lawama apewe makonda sasa hivi
 
Nakazia
 
Wasanii wengi Tanzania ni kula bata tu hawawekezi. Wachache wenye brains wako vizuri mfano the Commedy Group, WCB wakiongozwa na Diamond Platnumz etc. Yaani sina huruma na binadamu asiyejiwezesha. Baba wa Taifa alitufinza Ujamaa na Kujitegemea ili tusiwe ombaomba. Shida waliua Azimio la Arusha kupitia Azimio la Zanzibar mara alipofariki baba wa taifa hili. Tuache kutembeza bakuli. Ninamsifu mno Rais wetu wa Awamu ya tano Mh. Dkt JPM kwa kurudii kujitegemea. Sote tumuunge mkono maana amekataa kabisa kutembeza bakuli anakazania uwekezaji na mapato ya nchi hata kama kidogo tutumie hicho hicho. Kifupi SAHAU ombaomba. Hata harusi sasa na mazishi tujitegemee siyo kupitisha michango mpaka kwa third generation. AIBU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…