Msiba wa Rais Mkapa: Kwa nini Ubalozi wa UAE Tanzania haujashusha bendera nusu mlingoti?

... kwani mabeberu wakiongozwa na beberu mkuu nao wamepeperusha nusu mlingoti?
 
... umenena vyema! Ubalozi na eneo linalozunguka jengo la ubalozi kimsingi ni nchi ya kigeni na ndio maana hata mhalifu akikimbilia ubalozi wa nchi ya kigeni kuna taratibu za kumkamata kwani inahesabiwa yuko nchi nyingine.

Kwa hiyo mleta mada, usiwaingilie UAE (na nchi nyingine zote) na mambo yao. Wenye hiari ya kufanya hivyo watafanya kwa maelekezo kutoka nchi zao; wasiotaka (nchi husika) ni hiari yao pia wala sio kosa and in general huo msiba wala hauwahusu! Balozi zinazotakiwa kupeperusha nusu mlingoti ni balozi za Tanzania katika nchi za kigeni hilo linawahusu moja kwa moja.
 
Muongozo wanapata toka wizara zao za mambo ya nje. Watashusha kama kwao wakifiwa na serikali yao itasema washushe nusu mlingoti. Hawapokei maagizo toka wizara ya mambo ya nje ya tanzania.
... sawa sawa kabisa.
 
Jambo moja muhimu kujua ni kwamba, mahali palipo na 'jengo la ofili ya ubalozi' wa nchi yeyote panahesabika ni sehemu ya nchi hiyo. Hivyo basi ubalozini ni kama nchi: kushusha nusu mlingoti ni lazima uwe utaratibu wa nchi husika ndio umesikia kila palipo na ubalozi wa Tanzania washushe bendera nusu mlingoti.
 
Wapemba ni ndugu zao wa damu kabisa!
Umenikumbusha mbali sana enzi zie. Hawa jamaa walimtumia sana Komandoo kujaribu kumtikisa Mkapa wakati yuko mdarakani.

Walimchochea Komandoo na kumhadaa mpaka Komandoo akaiunga ZNZ kwenye jumuia ya nchi za kiarabu. Nakumbuka Mwalimu alikuwa hajafariki bado, Komandoo akapigwa mkwara na kupewa masaa 24 awe ameitoa ZNZ kwenye hiyo jumuia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Mwalimu alipofariki tu, Komandoo akatuma wazee wa ZNZ wamletee salamu Mkapa kuwa anabadili katiba, kufuta ukomo wa muda wa madaraka ili Komandoo aendelee madarakani. Tena kwa vitisho, Mkapa akigoma, ZNZ wanavunja muungano na kujiunga na UAE πŸ˜„πŸ˜„. Mkapa akasimama kidete.

Hao UAE wana roho kama za wajumbe wa CCM.
 
Ni lazima kushusha?
 
Kuteremsha bendera ubalozini ni nchi yake itangaze rasmi kuwa inaombeleza ndio balozi atateremsha bendera.mnakuwa mazwazwa hamuelewi kulaumu tuu
 
Labda sio taratibu zao, na kwani bendera yao inatuhusu nini?! Muwaache msijewaletea balaa bure.

Uko sahihi mkuu. Wakati mwingine ni vema kuachana na petty issues. Huyu jamaa hata kama UAE wangeshusha bendera, huenda angeuliza mbona serikali haikufunga sehemu za starehe kwa sababu ya msiba wa taifa!!
 
Umenena vema Mkuu. Tatizo tulilonalo ni maarifa na ujuaji
 
Itakuwa mpandisha bendera hajaambiwa labda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…