Watanzania,
Kama ambavyo pengine mmesha sikia, Mtanzania mwenzetu Ulimboka Mwaifuna amefariki dunia hapa Wichita.
Marehemu amefariki kwa ajali ya moto nyumbani kwake Jumapili alfajiri May 11, 2008. Kwa bahati, mke na watoto hawakuwepo nyumbani moto ulipotokea.
Marehemu alizaliwa 1978, na ameacha mke na watoto wawili, miaka 4 na miaka 2.
Zoezi linalofanyika sasa ni kuchanga na kukusanya pesa za kutoha ili tuweze kumsafirisha marehemu kurudi nyumbani Tanzania. Tunataka pia kumsafirisha mke na watoto ili waweze kuhudhuria mazishi.
Kwa kuwa nyumba ya marehemu imeungua, nguo za familia na vifaa ndani ya nyumba vimeteketea. Tunaomba watanzania ambao tunaishi hapa Wichita tuweze kukusanya na kuwasaiadia watoto kwa nguo na vifaa mbalimbali ili angalau tuwapunguzie mzigo huo katika kipindi hiki kigumu.
Account maalum imefunguliwa Bank Of America:
Account Number 518002076799.
Name of Acct ni Lunda Asmani.
Kutokana muda mfupi, hatujaweza bado kusajili Memorial Fund ya marehemu. Kwa wale tuliopo Wichita msiba upo nyumbani kwa
Abel Chamriho, 801 S. Christine.
Tunaomba kila Mtanzania atoe $100.00 (minimum), kabla ya Jumatano May 14, 9pm. Kule Tanzania wameshaanza msiba na macho yote yako kwetu sisi marafiki na ndugu tuliopo Marekani ili tuweza kumfikisha mwenzetu nyumbani Tanzania.
Kila siku kutakuwa na kikao saa tatu usiku ( 9pm) hapo msibani.
Tafadhali tunaomba kila Mtanzania ajiandikishe kwenye daftari la michango.
Nashukuru kwa ushirikiano wako.
Map and Directions
801 S Christine St
Wichita,
KS 67218-2635