Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Msichana mwerevu ambaye alifanya vyema katika Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) yuko kwenye hatari ya kukosa nafasi ya kujiunga na shule ya upili kwa sababu ya kuwa zeruzeru.
Winnie Jelimo, mwenye umri wa miaka 15, ambaye alipata alama ya 347 katika KCPE ya Machi, alisema ametembelea shule tano kutafuta nafasi bila kufua dafu.
Akizungumza na TUKO.co.ke, Jelimo alisema katika moja ya shule ambayo alitembelea, mwalimu mkuu alimwambia hawana nafasi ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.
"Mwalimu mkuu alimfahimsia baba yangu kuwa huwa hawakubali wato wenye ulemavu wa ngozi. Nilihisi uchungu sana, lakini baa yangu lijaribu kunitia nguvu. Sijawahi kubaguliwa kwa sababu ya hali yang hata nikiwa katika shule ya msingi," Jelimo alisema.
Ndoto zake zadidimia
Jelimo, ambaye alisomea katika Shule ya Msingi ya Ilula mjini Eldoret, alisema alikuwa anatumainia kujiunga na Shule ya Upili ya Chepterit katika kaunti ya Nandi na kufuata ndoto zake za kuwa daktari.
Lakini ndoto zake zinaendelea kudidimia kila siku. "Wenzangu wameteuliwa kujiunga na shule mbalimbali za sekondari, lakini nimewachwa nikijiuliza kwani nilikosea wapi kupitia haya,"
Read more: Mwanafunzi aliyepata 347 KCPE akataliwa na shule 5 kwa kuwa zeruzeru