Msichana wa 36 anasumbuliwa sana na Maumivu ya Kiuno. Afanye nini?

Msichana wa 36 anasumbuliwa sana na Maumivu ya Kiuno. Afanye nini?

MR.NOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
339
Reaction score
505
Wakuu kwema? Tunaomba msaada wa kitabibu/ ushauri ili huyu mwanamke apone. It's more than 5 years ila saiz hali ndio inazidi kuwa mbaya Zaidi, huyu ni binamu yangu analalamika kuumwa na kiuno na sehem ya chini ya mgongo. Ameenda hospital wanamwambia tatizo hilo limesababishwa na uzazi na kuanza kufanya kazi nzito baada ya kujifungua. Kama kuna mtu anafaham dawa/ tiba tunaomba atujuze tafadhali.Mwanamama huyu ana watoto wa tatu kwa sasa.
 
Ngoja kwanza, katika wasichana 37 wote hao huyo tu wa 36 ndio mwenye tatizo au katika mabinti zako hao wa miaka 2,5,8 huyu Bint yako wa miaka 36 ndio anatatizo?

Kama kuna maajabu kwa wasichana basi ajabu ya kwanza ni huu umri wa kuitwa kwake msichana.

Pole kwa binamu yako Nyama ya hamu.
Augue pole.
 
Wakuu kwema? Tunaomba msaada wa kitabibu/ ushauri ili huyu msichana apone. It's more than 5 years ila saiz hali ndio inazidi kuwa mbaya Zaidi, huyu ni binamu yangu analalamika kuumwa na kiuno na sehem ya chini ya mgongo. Ameenda hospital wanamwambia tatizo hilo limesababishwa na uzazi na kuanza kufanya kazi nzito baada ya kujifungua. Kama kuna mtu anafaham dawa/ tiba tunaomba atujuze tafadhali.
Ameolewa hana mwanaume?
 
Ngoja kwanza, katika wasichana 37 wote hao huyo tu wa 36 ndio mwenye tatizo au katika mabinti zako hao wa miaka 2,5,8 huyu Bint yako wa miaka 36 ndio anatatizo?

Kama kuna maajabu kwa wasichana basi ajabu ya kwanza ni huu umri wa kuitwa kwake msichana.

Pole kwa binamu yako Nyama ya hamu.
Augue pole.
Mtoto kwa baba hakuwi hata awe na miaka 50 atabaki kuwa binti! Jambo la msingi anaumwa kama kuna dawa unaijua mjuze jamaa!
 
Tatizo la kuzaa mtoto wa Kwanza umri ukiwa umeenda Sana.

Amshkuru Mungu, hajafa Wala hajaua mtoto anapojifungua.

Inatokana na nyonga kukakamaa Kama jiwe
Nyonga ikikakamaa Sana mtoto kupita Ni mbinde,ndo Mana wengi wanaopt kupigwa kisu.
Akilazimisha ananyonga mtoto au anakufa yeye mwenyewe.

Ndo maana inasisitizwa umri wa mwanamke awe ameshazaa Ni kuanzia 18-28 ambapo nyonga bado inakua flexible.

Ikizd hapo Ni kujitafutia MATATIZO ya uzazi Kama Uyo dada ako.

SOLUTION: Aanze kidg kidg kufanya kegel exercise tatizo litaisha lenyewe

POLE SANA MKUU
 
Wakuu kwema? Tunaomba msaada wa kitabibu/ ushauri ili huyu mwanamke apone. It's more than 5 years ila saiz hali ndio inazidi kuwa mbaya Zaidi, huyu ni binamu yangu analalamika kuumwa na kiuno na sehem ya chini ya mgongo. Ameenda hospital wanamwambia tatizo hilo limesababishwa na uzazi na kuanza kufanya kazi nzito baada ya kujifungua. Kama kuna mtu anafaham dawa/ tiba tunaomba atujuze tafadhali.Mwanamama huyu ana watoto wa tatu kwa sasa.
Kama ana miaka 36 na bado ni "msichana" dawa ni aondoke kwenye usichana awe mwanamke (aolewe).

Akitoka tu kwenye usichana tatizo lake litakuwa historia.
 
Ngoja kwanza, katika wasichana 37 wote hao huyo tu wa 36 ndio mwenye tatizo au katika mabinti zako hao wa miaka 2,5,8 huyu Bint yako wa miaka 36 ndio anatatizo?

Kama kuna maajabu kwa wasichana basi ajabu ya kwanza ni huu umri wa kuitwa kwake msichana.

Pole kwa binamu yako Nyama ya hamu.
Augue pole.
😂 😂 😂
 
Maumivu ya kiuno ni tatizo linalosumbua kwa watu wengi mara kwa mara. Katika makala hii tutaangalia zaidi tatizo hili kwa wanawake. Wanawake wengi husumbuliwa na maumivu ya kiuno. Hujitokeza mara kwa mara hasa wakati wa hedhi, na kisha kufifia. Kuna maumivu ya kiuno ambayo hukaa kwa muda mrefu mpaka miezi 6 na kuendelea au kuwa yanajirudia mara kwa mara kwa muda mrefu.

Maumivu haya huweza kusababishwa na matatizo kwenye via vya uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo mkubwa au misuli ya nyonga. Yanaweza kuwa yanaendana na mzunguko wa hedhi au la, huwa mara nyingi chini ya kitovu na kiunoni. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kuathiri shughuli zako za kawaida.

Sababu Za Maumivu ya Kiuno​

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ya kiuno kwa muda mrefu, sababu hizi ni:

  • Maumbukizi ya ndani ya kiuno ya muda mrefu (Chronic Pelvic Infection) kutokana bakteria wa magonjwa ya zinaa kama kisonono au wadudu wa TB.
  • Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ukuta wa uzazi huota sehemu nyingine za uzazi. Huleta maumivu wakati wa hedhi au kufanya mapenzi.
  • Maambukizi ya muda mrefu ya shingo ya uzazi au mji wa uzazi (Chronic endometritis or cervicitis). Husababisha maumivu ya kiuno wakati wowote na wakati wa kufanya ngono.
  • Vivimbe vya kizazi (uterine fibroids)
    Husababisha maumivu pale ambapo vinakua kwa haraka, vinajiviringisha au kukandamiza ogani nyingine. Maumivu yake huwa ya kuja na kuacha.
  • Maambukizi ya njia ya mkojo ya muda mrefu (Urinary Tract Infection)
    Husababisha maumivu hasa wakati wa kukojoa na chini ya kitovu.
  • Maambikizi ya via vya uzazi (Pelvic inflammatory Disease – PID)
  • Maambukizi ya Kibofu cha Mkojo (Interstitial cystitis)
    Hali hii huleta maumivu hasa chini ya kibofu cha mkojo ambayo hupungua pale unapokojoa. Dalili nyingine ni kukojoa mara kwa mara, kukojoa usiku na kushindwa kubana mkojo.
  • Ugonjwa wa Kidole Tumbo (Chronic Appendicitis)
    Tatizo la kidole tumbo huleta maumivu upande wa kulia chini ya kitovu ambayo huwa hayatulii na dawa za maumivu.
  • Kushikana KwaVia Vya Uzazi (Pelvic Adhesions)
  • Saratani ya Utumbo Mpana
    Tatizo hili huweza kuleta maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu na kiunoni kwa muda mrefu.
  • Ajali Maeneo Ya Kiunoni
    Ajali huweza kuathiri mifupa na mishipa ya fahamu iliyo maeneno ya kiunoni na hivyo kuleta maumivu ya kiuno ya muda mrefu.
  • Kusagika kwa Mifupa Kwenye Maungo (Degenerative joint disease)
    Mifupa ya kiuno huweza kuathiriwa na ugonjwa huu. Mifupa ya maungo ya kiuno inaposagika, husababisha maumivu makali maeneo ya kiunoni hasa wakati wa kutembea.

Matibabu​

Maumivu ya kiuno ya muda mrefu hutibiwa kwa kugundua chanzo cha maumivu kwanza. Kujua hili historia ya tatizo, uchunguzi pamoja na vipimo hufanyika.​

Matibabu hutegemea na chanzo cha tatizo; Dawa za kutuliza maumivu, dawa za majira kama tatizo linahusiana na mzunguko wa hedhi au upasuaji.
 
Tatizo la kuzaa mtoto wa Kwanza umri ukiwa umeenda Sana.

Amshkuru Mungu, hajafa Wala hajaua mtoto anapojifungua.

Inatokana na nyonga kukakamaa Kama jiwe
Nyonga ikikakamaa Sana mtoto kupita Ni mbinde,ndo Mana wengi wanaopt kupigwa kisu.
Akilazimisha ananyonga mtoto au anakufa yeye mwenyewe.

Ndo maana inasisitizwa umri wa mwanamke awe ameshazaa Ni kuanzia 18-28 ambapo nyonga bado inakua flexible.

Ikizd hapo Ni kujitafutia MATATIZO ya uzazi Kama Uyo dada ako.

SOLUTION: Aanze kidg kidg kufanya kegel exercise tatizo litaisha lenyewe

POLE SANA MKUU

Haahahhaahhaa...mkuu unayafahamu haya uloandika? Wanashauri umri wa kuzaa uwe mwisji 35..wengine wanashauri had 40..ila kegel excercise sio kbs na analoumwa..hahahaa kege ni.mazoez ya kurudisha uke ...elastic..lol...
 
Back
Top Bottom