Mhe Rais Magufuli, nakukumbusha kuwa kuna maazimio ya bunge ambayo hayajatekelezwa kuhusu kashfa ya escrow. Nayo ni haya yafutayo:
1.Kushitakiwa kwa Harbinder Singh Sethi kwa utapeli.
2. Kutaifishwa kwa mitambo ya IPTL kwa kuwa mauzo yalifanyika kwa kampuni hewa(isiyosajiliwa nchini) Pan Paper.
3. Fedha zote za escrow account zirudishwe na wahusika wote wafunguliwe mashtaka ya jinai na watumishi wote wa umma (pamoja na majaji) waliolipwa wachukuliwe hatua za kinIdhamu. Ni wakati muafaka wa kutumbua hili jipu pia.