Sawa mkuu!Watu wengi wamejaa fadhaa kutokana na mambo mbalimbali yanayoendelea huku na kule duniani: vita, magonjwa ya kutisha, ukosefu wa ajira, njaa, uhalifu, matetemeko, gharama kubwa za maisha, nk.
Rafiki, usifadhaike. Hayo yote karibu yatakwisha. Biblia inatuhakikishia kuwa hayo si maisha ya milele. Mungu anaumba dunia mpya isiyo na maovu, mateso wala huzuni.
“Sasa, naumba mbingu mpya na dunia mpya, mambo ya zamani hayatakumbukwa tena. Furahini, mkashangilie milele, kwa ajili ya vitu hivi ninavyoumba.."(Isaya 65:17)
Katika mbingu mpya na dunia mpya:
Hakutakuwa na machozi tena wala maombolezo au kilio. (Ufunuo 21:4)
Hakutakuwa na magonjwa wala mauti. Haki itatawala, na amani itakuwa ya kudumu.
"Lakini, kulingana na ahadi yake, twatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake."(2 Petro 3:13).
Hayo sio maneno ya kukutia moyo tu, ni ahadi za kweli kutoka kwa Mungu ambaye hasemi uongo. Kwahiyo tunapoona mambo yanazidi kuwa mabaya duniani, ni ishara kuwa mwisho wa mambo hayo umekaribia.
"Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia."(Luka 21:28)
Waebrania 10:23"Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia."(Luka 21:28)
Ameen, barikiwa sanaMsifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Yoh 14:1-4.
1 Wakorintho 1:18-31TRela tu hilo
Soma Biblia kwa makini. Jina “Wagalatia” linapatikana mara kadhaa katika Biblia, hasa kwenye waraka wa Paulo kwao — sio kama kabila, bali kama jamii ya kimataifa waliopokea Injili. Hii inaonyesha kwamba ujumbe wa Biblia haujafungwa kwa Wayahudi tu, bali upo kwa ajili yetu sote.Siku hizi mistari ya biblia imeanza kuniumiza macho yaan humo nakuta makabila ya wayahudi tu ila Wagalatia
WathesalonikeSoma Biblia kwa makini. Jina “Wagalatia” linapatikana mara kadhaa katika Biblia, hasa kwenye waraka wa Paulo kwao — sio kama kabila, bali kama jamii ya kimataifa waliopokea Injili. Hii inaonyesha kwamba ujumbe wa Biblia haujafungwa kwa Wayahudi tu, bali upo kwa ajili yetu sote.
Warumi 1:16
“Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye; kwa Myahudi kwanza, kisha kwa Myunani pia.”
Matendo 10:34-35
“Hakika natambua kwamba Mungu hana upendeleo, bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.”
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...Duh, unangoja uone kama yatakwisha?
Hesabu 23:19
Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize?