Msigwa Atoa Ufafanuzi Taarifa ya CAF Kuufungia Uwanja wa Mkapa, Kuhusu Derby Asema Waulizeni TFF

Msigwa Atoa Ufafanuzi Taarifa ya CAF Kuufungia Uwanja wa Mkapa, Kuhusu Derby Asema Waulizeni TFF

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa ametoa Ufafanuzi Taarifa ya CAF Kuufungia Uwanja wa Mkapa, Kuhusu Derby Asema Waulizeni TFF ambapo amesema ukaguzi ulipokuwa ukifanyika nyasi zilikuwa zimekatwa mpaka chini hivyo kupelekea kuchimbika baada ya mechi ya Simba SC dhidi ya Azam FC.

Hata hivyo amesema uwanja huo upo vizuri ni vema wakaguzi wakarudi tena kwani tangazo la ukaguzi limetolewa baada ya wiki tatu tangu ukaguzi ufanyike.

 
Kwa hiyo sasa wanazilaumu timu kwa kutumia uwanja? Eti pamechimbikachimbika kwa sababu ya mechi wakati huo huo anakiri mwenyewe kuwa hawakuwa na vifaa vinavyotakiwa kupunguza nyasi.

Dah mwanasheria wangu yupo bize na kesi nyingi, embu nisimuongezee mzigo.
 
Miaka miwili b30 hatuoni mabadiliko yeyote, kabla ya kutangazwa b30
Kuwa zitakarabati uwanja,uwanja ulikuwa katka hali nzuri na haukuwahi kufungiwa. Sasa uwekezaji na ukarabati wa uwanja kwa b30 umepelekea CAF waufungie kabisa.
 
Ziko wp bil 30 mlisema mtaweka viti vipya viko wp sasa pesa za watanzania hzo mlishagawana huko ccm au siyo.
 
Aachage Kurahisisha Vitu Muhimu
Atuembie Bl 30 mpaka sasa Kipi kimefanyika pale zaidi ya kufunga Tv na taa Ukiacha Mirangi!!
This country we have a very big curse..30 billion wasted like sperms , nothing useful has been done ..it's like you have give free money people to eat it.
 
Kweli Simba ni mtoto wa kambo. Kila lawama anapewa yeye.....
 
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharimu zaidi ya Sh. bilioni 31 hadi kukamilika Julai 2024.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam Julai 27, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chana baada ya kusaini mkataba na kampuni BCEG ya China ambao pia ndio waliojenga uwanja.

Maeneo yaliyopangwa yakarabatiwe ni pamoja na.
1. vyumba vya wachezaji,
2. chumba cha waandishi wa
Habari,
3.Eneo la watu mashuhuri (VVIP), 4. kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo,
5. ubao wa kuonesha matokeo,
kuweka mfumo mpya wa TEHAMA, kubadilisha eneo la kuchezea na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.

Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba,
7. mfumo wa umeme,
8. mfumo wa sauti,
9. Eneo la kukimbilia wanariadha,
10. chumba cha VAR,
11. lifti mbili mpya,
12. mfumo wa taa,
13. mfumo wa maji taka,
14. mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Wakaguzi wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) waliukagua Uwanja wa Mkapa, wiki mbili zilizopita lakini kwa sasa uwanja huo upo vizuri na tayari kutumika kwa kuwa marekebisho ya sehemu ya kuchezea yameshafanyika.

Mapema leo Machi 12, 2025 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilisema CAF imeufungia uwanja huo kutokana na eneo la kuchezea (pitch) kuendelea kupungua ubora wake ambapo Simba imetakiwa kuwasilisha jina la Uwanja utakaotumika kwa Mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri, Aprili 9, 2025.

Ili kuondoa usumbufu, TFF imetakiwa kutuma jina la uwanja mbadala utakaotumiwa na Simba kufikia Machi 14, 2025.
 
Back
Top Bottom