"Nimekuwa waziri kivuli wizara ya mambo ya nje, maliasili, kilimo. Kwa hiyo I know namna gani serikali inafanya kazi. Sasa, lakini kama haitoshi, wakati ule nafanya kazi tuko CHADEMA anaingia marehemu Magufuli, ambaye kwa namna fulani alikuwa tuna uhusiano naye, alinipa offer kubwa sana. Ningekuwa nataka cheo, ningekuwa nimeondoka siku nyingi sana CHADEMA nika... Na wote mliona Magufuli pale kule alitewa gari la ikulu lakini I just turned down.
Siwezi kuwajibia wengine, lakini kwa mtazamo wangu, siko driven na cheo. Kwa sababu ningetaka cheo kwanza, vyeo havipatikani CHADEMA. Pesa ziko CCM, vyeo viko CCM. Ungeamua, ningekuwa nataka cheo, ningeamua niwe napiga makofi. "Mama kaupiga mwingi, serikali inapiga mwingi", ningeendelea kusema hivyo ili walao naweza nikapata hata ukurugenzi au ukatibu kata.
Huku [CHADEMA] tunakomaa, ni msuli huku. Huku hakuna hela, unatafuta hela mwenyewe, unatumia gari lako mwenyewe, unapiga kampeni mwenyewe. Kwa hiyo mimi kinachonisukuma ni ile dhamira ya dhati, na ndio maana nimesema dhamira imenihukumu kwamba wito wangu mimi that's not my home, we are not compatible."