Msigwa: Ukiona hadi tumefika hatua kufungia chombo cha Habari, kuna mambo tukiendelea kuyaacha yataleta madhara kwa Taifa

Msigwa: Ukiona hadi tumefika hatua kufungia chombo cha Habari, kuna mambo tukiendelea kuyaacha yataleta madhara kwa Taifa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa ametoa sababu kwanini wanafikia hatua ya kufungia Baadhi ya Vyombo vya Habari

Soma Pia: Jambo Online TV wafungiwa kwa siku 90 na TCRA

Ukiona tumefikia hatua ya kufungia chombo cha Habari maana yake kuna mambo tukiendelea kuyaacha yanaletea madhara kwenye maslai kwa Taifa na kwenye usalama wa Taifa yanaivuruga nchi kwahiyo tusipochukua hatua hiyo hata sisi upande wa Serikali tutakuwa atutekelezi wajibu na tutakuwa hatutendi haki kwa Watanzania. Amesema Msigwa

 
Huyo bumunda aseme kwa nini Jamii Forum imefungiwia,
Atuambie JF imetishia maslahi gani ya usalama wa taifa
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa ametoa sababu kwanini wanafikia hatua ya kufungia Baadhi ya Vyombo vya Habari

Soma Pia: Jambo Online TV wafungiwa kwa siku 90 na TCRA

Ukiona tumefikia hatua ya kufungia chombo cha Habari maana yake kuna mambo tukiendelea kuyaacha yanaletea madhara kwenye maslai kwa Taifa na kwenye usalama wa Taifa yanaivuruga nchi kwahiyo tusipochukua hatua hiyo hata sisi upande wa Serikali tutakuwa atutekelezi wajibu na tutakuwa hatutendi haki kwa Watanzania. Amesema Msigwa

Wananchi hawatakiwi kuyajua maovu yenu wasije wakawaparua.
 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ameeleza kuwa serikali inaamini katika uhuru wa vyombo vya habari, akisisitiza kuwa tangu Rais aingie madarakani, alichukua hatua ya kuvifungulia vyombo vilivyokuwa vimefungiwa na kuvipa leseni ili viweze kuendelea na kazi zao. Hatua hiyo ililenga kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya serikali na wanahabari, kwa kuzingatia umuhimu wa vyombo hivyo katika maendeleo ya taifa.

Hata hivyo, amebainisha kuwa pamoja na uhuru huo, vyombo vya habari vimekuwa vikifanya makosa mbalimbali. Serikali imekuwa ikichukua njia ya mazungumzo na ushauri badala ya adhabu kali, kwa lengo la kurekebishana na kusonga mbele kwa pamoja. Msisitizo umewekwa katika kujenga uhusiano wa kuelewana badala ya kutumia nguvu za kisheria mara kwa mara.

Msigwa ameonya kuwa kufikia hatua ya kufungia chombo cha habari si jambo la kawaida, bali hutokea pale ambapo makosa yanahatarisha maslahi ya taifa au usalama wa nchi. Ameeleza kuwa iwapo makosa hayo yataachwa yaendelee, yanaweza kusababisha athari kubwa kwa jamii na hata kuchochea hali ya kuvuruga utulivu wa nchi.

Aidha, amekumbusha kuwa waandishi wa habari nao wako chini ya sheria kama raia wengine, na wanapaswa kuwajibika kwa matendo yao. Serikali inaendelea kusisitiza ushirikiano (engagement) licha ya kuwa na mamlaka ya kuchukua hatua kali, huku ikilenga kulinda maslahi ya taifa dhidi ya simulizi zinazoweza kulidhalilisha au kuligawa taifa.
 
Chivavilo mlimualika wenyewe Ikulu, picha mkapiga wenyewe mmevaa taulo, mkarusha mtandaoni wenyewe Kwa bando la serikali. JF waliporepost mkawafungia.
Wale Watangazaji wa Kyela FM wamesoma habari ilivyoandikwa na gazeti, mmeacha kukamata mhariri WA gazeti mmekamata aliyesoma gazeti, hizo akili au tope?
 
Back
Top Bottom