Comrade Mrisha
Member
- Nov 13, 2019
- 16
- 19
Uchaguzi ni mahesabu na hizo hesabu ndiyo ushindi wa Chama chochote kwenye uchaguzi. Hesabu na namba hazidanganyi. Kwa mujibu wa Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jumla ya Watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura ni 29,188,347 ambao hawa wataweza kupiga kura siku ya Jumatano Oktoba 28.
Kwenye idadi hiyo ya wapiga kura, CCM ina Jumla ya wanachama 17,000,000 ambao wote wamejiandikisha na wako tayali kupiga kura Oktoba 28. Ukiachana na hao milioni 17, CCM ina mtaji wa wafuasi wapya ambao wamejiandikisha hivi karibuni ambao ni milioni 5. Ukipiga mahesabu hapo jumla ya wapiga kura milioni 22 tayali ni wana CCM na hapo unagundua kabla hata ya CCM kuingia kwenye kampeni tayali alikuwa na ushindi mkononi wa zaidi ya asilimia 78. CCM inaingia kwenye ulingo huu kwenda kuzitafuta kura za watu milioni 7 pekee.
Sasa angalia hizo kura milioni 7 zinavyotafutwa kimahesabu na kisayansi ya kutisha. Piga mahesabu utekelezaji mkubwa wa Ilani ya CCM na ahadi zote, weka kampeni kubwa ya kistaarabu na kisayansi zilizojaa hoja, ushawishi na uhudhuriaji wa watu wengi ambazo zimepigwa na CCM kwa kuhusisha vinara watatu wakuu, Mgombea wake wa Urais Dkt John Pombe Magufuli, Mgombea mwenza Mama Samia Suluhu na mjumbe wa kamati kuu ndugu Kassim Majaliwa ambao waligawana nchi kwa kila mmoja kushambulia maeneo tofauti tofauti ya nchi ambako kote kumepigwa kampeni kubwa sana.
Hapo ongeza na timu nyingine ya viongozi wastaafu na waandamizi wa CCM ambao nao wamepita kila kona kusakanya kura. Wamepita kila sehemu kusaka kura ukilinganisha na vyama vingine ambao walikuwa wanashinda mitandaoni tu kupotosha na kusema watu.
CCM imeshawishi mamilioni kwa mamilioni ya Watanzania kuwachagua huku wakinufaika na mtaji wa kuwa na wanachama wengi wasanii wa kizazi kipya wenye majina makubwa ambao wanawatumia hao kwenye mikutano yao, jambo lililowavuta watu wengi zaidi kuhudhuria mikutano yao na hapohapo CCM ikatumia upenyo huo kupenyeza sera zake nzuri na kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Kumbuka vyama vyote vya upinzani havina mwenyekiti hata mmoja wa kijiji, mtaa na kitongoji anayeweza kuwasaidia kupiga kampeni huko chini ambako ndo kuna wapiga kura wenyewe, CCM huko kote ina wenyeviti wake, viongozi wa chama wa mashina, matawi, kata, wilaya na mkoa ambao wanasaka kura kila kukicha. Hakuna anayelala.
Mpaka sasa CCM imeshapita bila kupingwa kwenye majimbo 28 kati ya zaidi majimbo 264 na kata 850 kati ya kata 3957 ambako kwa tafsiri hiyo tu, maeneo hayo hayana tena wagombea wa upinzani wanaoweza kuwanadi wagombea wao wa Urais. Huko kote kumetawaliwa na CCM.
Kwa kampeni hizi kubwa za CCM maana yake zimewafikia zaidi ya wale wapiga kura milioni 7 ambao hawakuwa kwenye database yake huku ikijiimarishia kura zaidi kwa wapiga kura wake milioni 22 waliopo kwenye database yake na walio tayali kuipigia CCM.
Takwimu za utekelezaji wa mambo makubwa ndani ya miaka mitano tu ziko wazi, udhaifu wa vyama vya upinzani unaonekana. Nawakumbusha tu, wasije kusema wameibiwa kura ushindi wa kishindo na wa kihistoria ambao haujawahi kutokea toka mfumo wa vyama uanze unakuja. Tarehe 28 tu hapo.