KERO Msimamizi wa Jambo TV Online anachofanya sio kizuri kwa Tasnia ya Habari, anaumiza baadhi ya Vijana kisha anawatisha

KERO Msimamizi wa Jambo TV Online anachofanya sio kizuri kwa Tasnia ya Habari, anaumiza baadhi ya Vijana kisha anawatisha

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wengi hapa jukwaani natumaini tunafahamu chombo cha habari Mtandaoni cha Jambo TV, ni kati ya vyombo ambavyo vimekuwa vikifanya vyema kwa siku za hivi karibuni.

Pamoja na hivyo, lakini msimamizi wa chombo hicho amekuwa mwiba kwa baadhi ya Vijana wengi wanaopita kwenye chombo hicho na kuacha maumivu kutokana na vitendo vya udhalilishaji na ukiukwaji wa haki zao ambavyo amekuwa akiwafanyia.

Kuna Vijana zaidi ya 10 amewaachisha kazi ambapo aliwatoa kutoka Mikoa ya Nje ya Dar es Salaam, akiwaahidi maslahi zaidi, lakini akishawafikisha ofisini kwake baada ya kuwatumikisha kwa muda kwa ahadi za malipo, wanapoanza kumdai anawaachisha kazi bila kuwapa maslahi yao.

Kuna Vijana wawili waliondolewa ofisini hapo na kukosa sehemu ya kulala, hawakupewa stahiki zao, kibaya zaidi amekuwa akitoa vitisho kwao kuwa wakitoka kwenye ofisi zake wakihamia ofisi nyingine zilizoko Dar atahakikisha anatumia ushawishi wake kuwafanyia fitina na kuwaangusha.

Hivi karibuni kuna kijana mwingine alimtoa Mkoani, alipofika Dar na kufanya kazi kwa wiki mbili akamtimua na kumuondoa sehemu alipokuwa analala, kwa kuwa ‘dogo’ hakupewa stahiki zake amelazimika kulala Stendi ya Magufuli kwa siku nne huku akitafuta sehemu ya kujishikiza.

‘Bosi’ huyo anawaambia kuwa anaowaondoa ofisini kwa kuwa anafahamiana na viongozi wa juu Serikalini hivyo hawana pa kwenda kulalamika.

Mbali na hapo jamaa amekuwa akiwatolea lugha za udhalilishaji ikiwemo kuwatukana matusi yenye dhihaka na kejeli hasa wanaoanza kuomba malipo yao.

Baadhi ya Wanahabari wanaolalamika wamefikisha malalamiko yao Jumuiya ya Waandishi wa Mitandao ya Kijamii (JUMIKITA), ambapo amekuwa akionywa kirafiki kwa kuwa ana ukaribu na ofisi hiyo ambayo na yeye ni sehemu ya chimbuko la kuanzishwa kwake.

Natoa wito kwa Wizara, Habari Maelezo, Wadau wa Haki za Binadamu, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Baraza la Habari (MCT) kufuatilia kwa ukaribu madai hayo na kufanya uchunguzi kwa kuwahoji vijana ambao wengi naamini kwa mazingira waliyokumbana nayo wako tayari kutoa ushirikiano.
 
Mambo kama haya ni mengi sana tatizo watu wanaopelekewa malalamiko (wa serikalini) wanachukua rushwa. Mimi nilishapeleka issue kama hii na wakala chao ikaisha
 
Hii ni kweli kabisa huyo mkuria ni zaidi ya mtesaji halafu ni mtumia mabavu sana wengi wamekua wanakwazoka na tabia zake
 
Back
Top Bottom