LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi Karatu: Hakuna wagombea waliolazimishwa kujitoa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Karatu

LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi Karatu: Hakuna wagombea waliolazimishwa kujitoa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Karatu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Mambo ni moto, mi nawasogezea tu taarifa karibu, muda wa kufanya maamuzi ukifika mnakuwa na taarifa zote muhimu.

Kupata taarifa za mikoa mbalimbali kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024


Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha Bw. Juma Hokororo amesema taratibu na kanuni zote za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 zitazingatiwa kikamilifu na hakuna kanuni zitakazovunjwa au Chama ama Mgombea yeyote atakayedhulumiwa haki yake ya Kikatiba kwenye Uchaguzi wa Novemba 27, 2024.

Hokororo ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Novemba 02, 2024 baada ya jana Ijumaa kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambapo Moja ya Chama cha siasa kinachoshiriki katika uchaguzi ujao kudai kuwa wagombea wake wawili wamejaziwa fomu za kujitoa kwa lazima katika uchaguzi na watu wasiojulikana.

“Kama msimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi katika maeneo ambayo wagombea hao wamechukua fomu, hatujapokea fomu yoyote ama barua za kujitoa kwenye uchaguzi kwa viongozi hao.” Amesema Bw. Hokororo.

Katika hatua nyingine msimamizi huyo wa uchaguzi amewaambia wanahabari kuwa Ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ipo wazi muda wote, akiwakaribisha wanasiasa na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwasilisha changamoto ama vikwazo wanavyokutana navyo kwenye mchakato wa uchaguzi huo wa serikali za mitaa.
 
Kanuni na MAELEKEZO kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Je, tunatakiwa kufuata Sheria na Kanuni za Uchaguzi au hayo MAELEKEZO kutoka OR-TAMISEMI?
 
Back
Top Bottom