Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Kama vile imekuwa mashindano kuangalia wapi wataengua waombea wengi kuliko wenzao!
=====
Jumla ya wagombea 350 wa nafasi mbali mbali za uogozi wa Serikali za Vijiji na Vitongoji wameenguliwa kati ya 4,282 ya waliochukua fomu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara Bw.Abeid Abeid Kafunda mara baada yakuzungumza na Safari Media ambapo amesema kuenguliwa huko kumetokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutofikisha umri wa miaka 21 ambao upo kikanunu vilevile kutokujua kusoma wala kuandika na kutokuwa na shughuri rasmi.
Aidha Kafunda amesema amesikitishwa kwakua na idadi kubwa ya watu walioenguliwa licha ya kutolewa elimu kwa makundi yote juu ya ujazaji fomu kwa kuzingatia miongozo,kanuni na taratibu.
Ameendelea kueleza sababu zilizowafanya viongozi hao kuenguliwa kwa idadi kubwa na namna hiyo kwa kutokana na kukiuka kanuni na sheria za uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutokidhi vigezo.
"Wapo walioenguliwa kwenye nafasi ya uongozi kwakua tu shughuri zao zilikuwa na maslahi ya moja kwa moja na serikali ya sehemu husika au serikali kuu mfano baadhi ya viongozi wakandarasi kwenye majengo yetu,wana mikataba na halmashauri sheria inasema kabla hujajaza fomu lazima ueleze wazi kwamba wewe una mkataba kwahiyo watu wameondolewa kwa haki hakuna aliyeonewa."Amesema Kafunda