Msimamo mbovu wa serikali utatuingiza vitani

swagazetu

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
4,250
Reaction score
1,470
Kwa hakika nchi yetu Tanzania tunaipenda lakini mahali na hali tuliyofikia ni mbaya.

Swala la vita tumeanza kulizungumza kama utani utani kama mtu na mkewe chumbani.serikali nayi msimamo wake umekuwa wa utani haiangalii nini tatizo viongozi wanatoa propaganda na kupinga vikali bila hatua yoyote kuchukuliwa.hakuna anaekemea majibu ni mepesi sana hayana suluhisho.

Msimamo wa serikali yetu juu ya matukio mbalimbali ni mbovu na kwa sababu ya kushindwa kuchukua hatua imebaki kutupia lawama cdm au cuf hatua hazichukuliwi.

Kama wauwaji ni chadema mbona serikali haichukui hatua dhidi yao?matukio ya utekaji na uteswaji wa akina ulimbika,Absalom kibanda,Saed kubenea na wengine tuliambiwa na baadhi ya viongozi eti wanahusika chadema mpaka leo hajakamatwa yeyote wa chadema! Je chadema wako juu ya sheri?au ni propaganda hawahusiki? Mimi naomba tujiulize kama serikali itaendelea na msimamo ea kutupiana mpira hatutaingia vitani?kama chadema au cuf wanahusika basi sheria ichukue mkondo wake vinginevyo itafikia wakati tutaamini kuwa serikali inawalinda wahalifu wa vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani.

kifo cha mwangosi tuliambiwa na serikali chadema wanahusika!hakuna aliyekamatwa wala kuhijiwa kutoka chadema!

Kuteswa kwa Absalom kibanda tukaambiwa na wanasiasa wa ccm chadema inahusika!hakuna aliyekanatwa kutoka chadema!

Kuvamiwa na kuuawa kwa Dr mvungi yumeambiwa ni wahuni tu!

Kama chadema wanahusika je wako juu ya sheria? Au serikali inawajua wahalifu?hii ni kwa sababu kwa namna chadema inavyosakamwa kweli wangefanya haya wangesalimika au wangefutiwa hata usajiri!

tujue kuwa maeneo vita ilikotokea sababu hazikuwa kubwa wakati mwingine ni hata zilizodharaulika sasa serikali yetu acheni kurushiana mpira washughulikieni tuepeke vita.
chadema wanasisitiza ktk mikutani yao kuwa watekaji na watesaji wafhukuliwe hatua sasa kweli kama mhalifu anaomba achukuliwe hatua serikali inaogopa nini?
 
Mkuu, vita kati ya nani na nani? Kama CHADEMA mnajifariji kuwa mtapambana na serikali, huko ni kuwehuka. Tulimpiga Idd Amin Nyumbani kwake. Sitashindwa nyie mburulaz?
 
Mawazo ya kijuha kabisa haya. Nani aingie vitani? Kama mnajidanganya kuwa kwa kutoboa watu macho kwa bisibisi ndo vita, hakika mnajidanganya
 
Tatizo la watanzania hatukubali ukweli na uongo utatufikisha pabaya.so wewe hutaki serikali ichukue hatua!kila msema kweli ni chadema!akili mbovu!
 
tujue kuwa maeneo vita ilikotokea sababu hazikuwa kubwa wakati mwingine ni hata zilizodharaulika sasa serikali yetu acheni kurushiana mpira washughulikieni tuepuke vita.
chadema wanasisitiza ktk mikutani yao kuwa watekaji na watesaji wafhukuliwe hatua sasa kweli kama mhalifu anaomba achukuliwe hatua serikali inaogopa nini?

..............
 
Tatizo la watanzania hatukubali ukweli na uongo utatufikisha pabaya.so wewe hutaki serikali ichukue hatua!kila msema kweli ni chadema!akili mbovu!
Na ikichukua hatua bado mtaendelea kulalamika na kujambajamba tu. si umeona jinsi mlivyoishambulia kuhusu operesheni tokomeza? Wengi waliopiga kelele hawakuchukia yaliyotokea wakati wa operesheni hiyo bali walikuwa hawaitaki kabisa
 
Mkuu, vita kati ya nani na nani? Kama CHADEMA mnajifariji kuwa mtapambana na serikali, huko ni kuwehuka. Tulimpiga Idd Amin Nyumbani kwake. Sitashindwa nyie mburulaz?
si watasaidiwa na kagame,pia ujerumani.
 
Kama akina Kasulumbai wametoboa mtu macho,kama akina Kilewo wamemwagia mtu tindikali kule Igunga, kama Mbowe alimuua chacha wangwe na nyie mnaonifanya mnauchungu sana baco mmekaa kimya!
 
Kama nanii alimfunga milele Babu Seya je.....
 
Na ikichukua hatua bado mtaendelea kulalamika na kujambajamba tu. si umeona jinsi mlivyoishambulia kuhusu operesheni tokomeza? Wengi waliopiga kelele hawakuchukia yaliyotokea wakati wa operesheni hiyo bali walikuwa hawaitaki kabisa

Wale 40 JK aliosema anawajua walikamatwa wakati wa operesheni tokomeza?ama ni nani alilengwa katika operesheni hii?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Anayehusika na mauaji ya watu ni ccm na serikali yake, ukiwa mpinzani kwenye hii nchi, jambo la kwanza ni lazima uwe msafi, kwa sababu serikali ya ccm haiwezi kukuacha, itatumia mwanya huo kuwafutia usajili, kama CHADEMA chama cha wananchi, kingekuwa kinahusika na haya mambo machafu, nakuhakikishia, leo hii kisingekuwepo, wewe huoni walivyotengeneza kesi ya ugaidi ya Lwakatale, lengo lilikuwa ni kutafuta njia ya kuifutia Chadema usajili, lakini walikwama, je! Kama kweli Chadema wanahusika, wangepona? Wanaohusika ni wakina Igondo Ramadhan usalama wa taifa pale ikulu, walitajwa na ----------- likangiwa, wengine ni Mwigulu Nchemba, Emmanuel Nchimbi, IGP mstaafu Said Mwema, Kamhando aliyemuua Mwangosi Iringa, rejea email zilizokamatwa baada ya kifo cha Dr Sengondo Mvungi, kati ya Mwigulu Nchemba na Emmanuel Nchimbi, na Zitto akihusishwa kuiua Chadema.
 
Kikwete amewahamasisha wanaCCM wote wajiandae kuwapiga wanachama wa vyama pinzani.
 
Mh!
Mbona kama wadau mnatoka nje ya mada!
Mtoa mada yupo sahihi!
Ni wehu chama na serikali kutaja wahusika,na kutowakamata..
 
Anayehusika na mauaji ya watu ni ccm na serikali yake, ukiwa mpinzani kwenye hii nchi, jambo la kwanza ni lazima uwe msafi, kwa sababu serikali ya ccm haiwezi kukuacha, itatumia mwanya huo kuwafutia usajili, kama CHADEMA chama cha wananchi, kingekuwa kinahusika na haya mambo machafu, nakuhakikishia, leo hii kisingekuwepo, wewe huoni walivyotengeneza kesi ya ugaidi ya Lwakatale, lengo lilikuwa ni kutafuta njia ya kuifutia Chadema usajili, lakini walikwama, je! Kama kweli Chadema wanahusika, wangepona? Wanaohusika ni wakina Igondo Ramadhan usalama wa taifa pale ikulu, walitajwa na ----------- likangiwa, wengine ni Mwigulu Nchemba, Emmanuel Nchimbi, IGP mstaafu Said Mwema, Kamhando aliyemuua Mwangosi Iringa, rejea email zilizokamatwa baada ya kifo cha Dr Sengondo Mvungi, kati ya Mwigulu Nchemba na Emmanuel Nchimbi, na Zitto akihusishwa kuiua Chadema.

Mwanamakambako natamani uanzishe uzi unaohusu hizo e mail kuhusu dr mvungi.
 
Kikwete amewahamasisha wanaCCM wote wajiandae kuwapiga wanachama wa vyama pinzani.
Watatwangwa tu ikiwa watatuchokoza. Ile tabia ya kugeuzia shavu la upande wa pili unapopigwa tumeikataaa na mwenyekiti wetu ametuambia kabisaaaa tusiwe wanyonge
 
Ni nani alie/anaewachokoza?
Ile kauli ni ya kipuuzi sana! Nikauli ya kutolewa na wavuta bangi vijiweni!
...
Kama mnapigwa si kuna mahakama, kwanini msipeleke kesi zenu mahakamani?
 
Back
Top Bottom