Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Lengo la chama cha upinzani ni kupata wabunge wengi ambao hawana athari zozote kwa chama tawala? Yaani ukipata wabunge 40 au 60 bado unafikiri umefikia lengo... labda uliangalie lengo hasa ni nini.
 
Lengo la chama cha upinzani ni kupata wabunge wengi ambao hawana athari zozote kwa chama tawala? Yaani ukipata wabunge 40 au 60 bado unafikiri umefikia lengo... labda uliangalie lengo hasa ni nini.
Ni kwanini shabiki wa Yanga unalia sana na kupigania Kocha wa Simba ajiuzulu??

CCM wote mko obsessed na Mbowe.

Kama wabunge 60 wa upinzani hawana athari kwa chama tawala ni kwa nini mmepiga marufuku vipindi vya bunge live??

Kama wabunge 60 wa upinzani hawana athari kwa chama tawala kwani mmepiga marufuku shuhuli zote za mikutano ya kisiasa hadi wabunge wa upinzani wakitaka kufanya mikutano mnaweka mazuiyo kwa kisingizio cha intelijesia hewa?

Kama wabunge 60 wa upinzani hawana athari kwa chama tawala kwanini CCM inatumia mabilion ya fedha kuwanunua wabunge wa upinzani wa maeneo wanayoona CCM haina nguvu ya kushinda hata kwa goli la mkono?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunataka TUME HURU YA UCHAGUZI. Msitutoe kwenye mstari. Ikiwepo tume huru hapo sasa ndipo upime uhalali wa viongozi wa upinzani
 
Yaani wapinzani wa CDM..mujifanye washauri wa Mbowe si ni Uchawi wa mchana huu??
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lako au tatizo lenu mafisiem hamtaki kusikia wala kumwona mtu mwenye akili na msimamo.Huyu Mkiti sisi tunamkubali na wewe hutakaa wala hutaweza milele kutuchagulia kiongozi.Kama umetumwa na Musiba,kamwombie hujatukuta mlango ulikuwa umefungwa na kofuli.Labda rudi kesho.
 
Hii nchi ina wajasiriasiasa wengi wanaojiita wanasiasa.
 
Kama Wewe pia ni msomi ktk Taifa letu,basi wasomi mmekuwa mstari wa Mbele sana kuliaibisha Taifa letu.kama ni laana ktk Taifa basi watu wa kwanza kupata laana mtakuwa nyinyi wasomi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma bila kuweka hisia zilizoumizwa. Unaona bado anastahili kuongoza CHADEMA kuelekea kushindwa tena? Hadi nini kitokee ndio utajua upinzani unahitaji kiongozi mwingine?

..hebu define " kushindwa " kwanza.

..kwasababu kuna wengine wanaamini tangu Mbowe amekuwa mwenyekiti chama kimekuwa kikikua kwa kuongeza idadi ya mashabiki, wanachama, na wabunge.

..pia ubora na udhaifu wa Mbowe unaupima vipi? Unamlinganisha na wenyeviti waliopita wa CCM? Au unamlinganisha na wenyeviti wa vyama mbalimbali vya upinzani nchini? Au unajaribu kuona ni wapi angeweza kufika, lakini hakufika, kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa na resouces at the disposal of his party?

..kwa CDM what is realistic and unrealistic when we are discussing victory in an election. Ni matokeo gani tunaweza kusema wame-underachieve, au wame-exceed expectations.

Cc Mag3, Nguruvi3, Erythrocyte , Pascal Mayalla
 
Wangelikatiwa ruzuku ili vyama viendeshwe kwa michango ya wanachama, hivi vyama vya kihunihuni vingelijichuja vikafa bila kupigiwa kelele na mtu.

Lakini hii ruzuku ya mamilioni, mtu anaficha aibu zake mgongoni, maana akiisha ukwaa uenyekiti, ashinde asishinde kwake ni ulaji, ndiyo maana wanang'ang'ania kwa mbinu chafu na vitisho kama manyang'au kwenye mzoga.

Wapo hapo kwa ajili ya maslahi ya matumbo yao na si kwa maslahi mapana ya watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana; mawazo yako ndiyo yanaitaji mjadala siyo ya MMK. Mwenyekiti Mbowe anatakiwa kuchirewa graph kuonesha kua amepandisha chama au amekishusha. Na pia inatakiwa tuchoro graph ya mafanikio ya wenyeviti wote wa vyama vya siasa nchini ili kuona wanafaa kuendelea au lawama kwa wale ambao walishamaliza muda wao.

Kwa mawazo yako Mwanakijiji ni nani anaweza kuwazoia mwanachama kutoka ndani ya chama kwa mapenzi yake?
 
Kwa mawazo yako ndugu ungetusaidia ni yapi ya kihunihuni ambazo msajili wa vyama vya siasa bado anavifumbia macho?
 
Soma bila kuweka hisia zilizoumizwa. Unaona bado anastahili kuongoza CHADEMA kuelekea kushindwa tena? Hadi nini kitokee ndio utajua upinzani unahitaji kiongozi mwingine?
Sikiliza ww nyumbayako inaungua unaenda kuzima moto kwa jirani ww VP siunachama chako cha ccm kinacho wabambikizia watu kesi ,kinachowapiga watu risasi kinacho muogopa maalim seif kinacho zuia mikutano ya siasa kinacho teka watu na kuwatia ktk viroba sasa kama unaushauri washauri ccm hayo mambo waachane nayo siyo uishauri upinzani kwani nyinyi hamuna mawazo mazuri kwa upinzani nyinyi mwataka wapinzani waharibikiwe mufurahi tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msiwauzie chadema hili lengo kutu; kwamba upinzani upimwe kwa watu wanavyoshangilia, kwa watu kupiga kura bila kushinda n.k. Kama hili ndio lengo la upinzani basi watu warithike tu na MBowe hadi watakapokuwa na lengo linaloeweka kweli kweli.
 
Huyu jamaa bhana
Si uanzishe chama chako sasa.... mbona kwa muda mrefu sana umekuwa CCM na unaunga mkono ukandamizwaji wa upinzani nakusheherekea udhalimu wa demokrasia kwa kisingizio cha maendeleo. ...

Why don't you give it a try... MMM Party
Binafsi sipendi viongozi kuhodhi madaraka kwa muda mrefu, lakini sijioni kama nina haki ya kumwambia Mbowe ajiuzulu.

Kwa sababu mimi si mwanachama wa CHADEMA.

Wanachama wa CHADEMA ndio wenye haki ya kuamua wawe na mwenyekiti wa maisha au wawe na term limits.

Sasa Mzee Mwanakijiji wewe ni mwanachama wa CHADEMA?
 
..hebu define " kushindwa " kwanza.

Kama umenisoma hapo juu utaona kuwa kushinda maana yake "kushinda uchaguzi na kuchukua madaraka".
..kwasababu kuna wengine wanaamini tangu Mbowe amekuwa mwenyekiti chama kimekuwa kikikua kwa kuongeza idadi ya mashabiki, wanachama, na wabunge.

Wenye kufikiria chama kinapiwa kwa wingi wa wanachama na kuwa ukiwa na wanachama wengi lakini hushindi uchaguzi basi ni vizuri hawajui maana ya siasa za upinzani.

Nimeshajibu hapo juu; vinginevyo nitakuwa najirudia rudia kama pia.
..kwa CDM what is realistic and unrealistic when we are discussing victory in an election. Ni matokeo gani tunaweza kusema wame-underachieve, au wame-exceed expectations.

Cc Mag3, Nguruvi3, Erythrocyte , Pascal Mayalla

Mkuu mwenzangu huo ni utani...
 
Msiwauzie chadema hili lengo kutu; kwamba upinzani upimwe kwa watu wanavyoshangilia, kwa watu kupiga kura bila kushinda n.k. Kama hili ndio lengo la upinzani basi watu warithike tu na MBowe hadi watakapokuwa na lengo linaloeweka kweli kweli.
Sometimes tuwe realistic; kipindi cha ukoloni ilituchukua muda mrefu sana kupigania uhuru adi tukaupata. Kwa mazingira yalivyo kuhusu sheria..tume ya uchaguzi na muunganiko.wa organs zote siyo rahisi kwa chama cha siasa kushinda uchaguzi ki urahisi na ndiyo maana CDM wamepiga hatua kubwa.

Sisi wananchi maisha yetu tumewaacha wanasiasa waamue na tunaona kabisa sheria na katiba zinakanyagwa lakini kondoo nyie kichwa chini mkitegemea Mbowe ndo awapiganie.
 

..labda mwenzetu unataka ARMED STRUGGLE.

..sisi wengine hatutaki kabisa kusikia habari hiyo ktk ardhi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…