HNIC
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 1,898
- 2,197
Hawa ndio Viongozi wa baraza kuu la waislam lililoanzishwa na Serikali ya CCM wakiongea na waandishi wa Habari
Kwa waislam simaanishi ile NGO iliyoanzishwa na serikali ya CCM kuwawakilisha waislam inayoitwa BAKWATA ambayo viongozi wake hakuna hata mmoja aliyesoma sekondari. Bali nazungumzia jumuia zingine ambazo ziko independent from Govt ambazo viongozi wake ni makini na wanawakilisha maoni ya waislam wengi zaidi Tanzania.
Naamini kuwa waislam wa Tanzania wana issues nyingi zaidi ya Mahakam ya Kadhi, Na pia najiuliza kuwa kama Wakristo makini Tanzania mawazo yao yashawasilishwa na TEC sasa naamini ni zam ya waislam na ikiwezekana Viongozi wa Dini zote 2 waungane kutoa msimamo thabiti kwa waumini wao juu ya hii kura ya maoni.
Naamini waislam hawajasahau jinsi walivyotumiwa na CCM kwenye kura za uchaguzi 2010 na pia nilifurahishwa walivyofanya hima na kugoma kuhesabiwa kwenye sensa sasa sioni washindwe vipi kujimobilise na kutumia lobby groups zao kushinikiza CCM juu ya interests zao kama ambavyo TEC walivyofanya.