Msimamo wako kiuchumi ndio fursa yako

Msimamo wako kiuchumi ndio fursa yako

john issa

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2017
Posts
856
Reaction score
1,638
*HEBU TUONGEE KIBIASHARA SASA:*

Ukipata nafasi ya kufika kule *Mbozi Mbeya*, ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na *kilimo cha kahawa*, kwa kweli unaweza kuhweuka, na kujiona kama mtu uliechelewa kweli kweli.

Wakati unarudi, kama ukishuka *Mafinga* na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na *biashara ya miti na mbao*, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!

Ukitoka pale ukaenda mpaka *Mang'ula na Ifakara Morogoro*, ukakutana na habari za watu *wanavyopiga hela kwenye mpunga*, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, "Nilikua wapi siku, zote hizi?"

Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi *Kariakoo*, kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule *China, Uingereza na Dubai*. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi. Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kufight kupata fremu pale!

Usiende kwanza *Zanzibar*, bali chukua Fastjet uende chapchap kule *Arusha*. Hapo kutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji. *Ukisimuliwa ABC za madini* na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana!

Unapoendelea kutafakari, *rudi mtandaoni*. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa *Network Marketing* utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua mavouge yao, *wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata Dubai, Paris, Madagascar na Uamerikani*, nakwambia korosho utaziona takataka.

Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mipunga ya Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, *usiombe ukutane na fursa ya digital currency*, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua.

Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale *tunaokinadi kilimo kama dhahabu* inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda! Ngoja *niuchune kukupeleka kwenye fursa ya samaki* kuzitoa Mwanza kupeleka Congo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!

*KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:*

1. Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.

2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri. Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k. Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.

3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Ashura. Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa. Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya networkmarketing, lakini mwingine nature ya network marketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwneye mbao, mwaka mmoja mbali unaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.

Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung'ang'ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover katika networkmarketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna, kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye Kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umejenga. Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!

4. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka. Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua. Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.

5. Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi, na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingine atasema kuanzisha kanisa kuna lipa....mbn gwajima kanunua ndege.........my friends tuliza moyo wako hapa twapita..........unaweza kuona frusa na kuanza na mtaji kidogo maybe wa laki 1, mwingine akaanza na m1, ajabu wew wa lak ukapaa huyu wa million akashuka......frusa ni akili yako tuuu........hata biashara ya karanga za kupima inaweza kukufanya uwe billionaire.............Uzi bora wa mwaka kwenye jukwaa la biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu kubwa ya biashara ulizotaja zina siri wamekueleza kama huko mbeya utasikia kaua mama yake au mwanawe wamekueleza changamoto zake wamekupa wewe umeysikiliza mafanikio tu ukaleta uzi kama rahisi rahisi tu
Mkuu sijabahatisha mkuu mm menyewe Wa mbeya! Naongelea kitu ninachokifanya mm mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi umesimama kwelikweli. Nadhani Changamoto kubwa ni katika kujua ni fursa ipi ya kuendelea nayo na ipi uachane nayo yaani kujua fursa sahihi kwako. Mbaya zaidi unakuta umeshaianza umepoteza fedha na muda kwahiyo kuiacha inakuwa mtihani

Embu tujadili ni namna gani utajua kuwa fursa fulani ni sahihi kwako? Na namna gani utajua kuwa unatakiwa kuiacha fursa ambayo umesha ianza kwasababu sio sahihi kwako
 
Uzi umesimama kwelikweli. Nadhani Changamoto kubwa ni katika kujua ni fursa ipi ya kuendelea nayo na ipi uachane nayo yaani kujua fursa sahihi kwako. Mbaya zaidi unakuta umeshaianza umepoteza fedha na muda kwahiyo kuiacha inakuwa mtihani

Embu tujadili ni namna gani utajua kuwa fursa fulani ni sahihi kwako? Na namna gani utajua kuwa unatakiwa kuiacha fursa ambayo umesha ianza kwasababu sio sahihi kwako
b7f6829747cd67554725a68ac295bad5.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja kwa nukuu moja ya Warren Buffet - “You only find out who is swimming naked when the tide goes out.” Kwenye ujasiriamali kukitokea changamoto ndiyo hasa utajua nani ni mkulima na nani ni mpiga mahesabu ya keyboard mzuri.
 
tatizo nitajuaje sasa kama hiyo kazi ndio ninayostaili kuifanya maana hamna kazi kama kuchagua aina ya kazi ya kufanya inauma sana haisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niishie tu kusema asante,kwasababu siwezi kueleza jinsi ulivonigusa,nmejifunza kitu kikubwa sana,kwangu huu ni uzi bora kuliko nyuzi zote nilizosoma JF 2017,keep it up brother.
Nakuunga mkono kwa asimilia nyingi. Nyuzi km hizi zinanifanya nisijutie kuwa mwana jf. Jamaa kaanindika kitu ambacho most of people tukistick kwacho mafanikio itakuwa ni sehemu ya maisha yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom