Msimamo wangu kuhusu ilani ya siku30 ya kutaka nilipe fidia ya 200ml

Msimamo wangu kuhusu ilani ya siku30 ya kutaka nilipe fidia ya 200ml

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
1,234
Reaction score
1,815
Ndugu wanaJF
Mtakumbuka siku ya jumamosi tarehe 2.4.2011,nilieleza jinsi nilivyomkamata na kumpeleka kituo cha polisi wakala aliyekuwa anakusanya ushuru wa maegesho ya magari kwenye kituo cha kuratibu safari za kwenda kwa babu,kinyume cha sheria
Jana asubuhi nilikuta ilani kutoka kwa mwanasheria wa huo wakala ikikusudia kunipandisha kizimbani baada ya siku 30,kudai fidia ya 200mil,kwa kuharibu mali,kuwadhalilisha,na kuwapeleka polisi kinyume cha sheria
MSIMAMO WANGU.Ninaamini kwenye kile nilichokifanya na nitayasimamia maamuzi yangu,kimsingi nimemtaka aende MAHAKAMANI;na tukutane huko,lakini pia akihitaji mchango ili aweke jopo la mawakili nipo tayari kumchangia
Nimechagua kutokuogopa na kamwe sitishwi,wala sitaogopa kutetea maslahi ya wananchi,
nawasilisha
Nanyaro
 
Kabla ya kuchangia nipe thread hiyo ili niipitie kisha tuwasiliane mkuu,
 
Mkuu wasikutishie nyau. Mbele kwa mbele mahakaman, hakuna kuogopa kama wanataka mil200 waende kwa EL, RA na mwezao zitto K
 
umeongea kwa jazba sana. Wengine hatujapitia hiyo thread yako ya awali.
Tupe summary ilikuwaje.
 
mkuu hebu tutupie iyo thread ya kwanza then tujue tunajibu vip hi siredi
 
Back
Top Bottom