Parody
Member
- Sep 13, 2020
- 24
- 69
Wakuu, nawasalimu kwa Jina la Jamhuri.
Nimepita mitandaoni, nimeona jinsi watu wanavyomshambulia Mwigulu kuhusu tozo ya miamala. Naunga mkono mashambulizi, lakini nadhani tunakosea tunayemwelekezea mashambulizi hayo.
Wanasema kila zama na kitabu chake. Wakati wa enzi za Mwendazake, taifa lilikuwa na ajenda ya kuondoa hofu kuhusu corona, na moja kati ya njia zilizotumika ni kuhakikisha ugonjwa wa corona unaonekana si lolote, na kuwa umeletwa na mabeberu, na kuwa hii ni vita ya kiuchumi.
Sasa, ili kufanikisha ajenda hiyo, ilibidi apatikane mtu atakayeongoza mapigano kwa niaba ya Mwendazake. Chaguo la kwanza lilikuwa Dkt. Ndugulile kwa kuwa alikuwa Waziri wa Afya. Kwa jinsi ninavyomfahamu, Dkt Ndugulile ni daktari kwa taaluma, na anawajibishwa na kiapo chetu cha Hippocratic Oath. Asingeweza kuupotosha umma kwa maslahi ya kisiasa. Na hicho ndicho alichokifanya. Kwa kuwa alionekana hawezi kutekeleza maagizo, ikabidi apaki pembeni.
Akaletwa mama yetu. Picha la kwanza, kaanza na scarf za bendera ya Tanzania (Naanza kuwa na wasiwasi na hawa wanaovaa scarf na tai za bendera maana Mwigulu naye humohumo 😁). Maelezo yasiwe mengi, tunajua alichokifanya. Sasa zama za Mwendazake zimepita na kitabu chake (ingawa bado tunaendelea kuisoma namba kwenye kitabu hicho). Zimekuja zama za Kazi Iendelee.
Mtazamo wangu ni kuwa ajenda ya zama hizi kwa sasa ni kuhakikisha mjadala wa katiba mpya unazimwa kwa nguvu zote, na ili kufanikisha ajenda hiyo, lazima litafutwe jambo zito litakalowaondoa Watanzania kwenye kujadili katiba mpya. Jambo lenyewe ni Kodi ya kipumbavu inayomgusa mwananchi moja kwa moja.
Mnakumbuka hadithi ya Sungura na jogoo wa baba? Jinsi sungura alivyofanikiwa kumtupia mbwa mifupa ya jogoo ili apate mwanya wa kutoroka? Ndicho kinachofanyika sasa. Mwigulu anatumika tu kama scapegoat na anafuata tu maelekezo. Suala la tozo ya miamala ni kubwa kuliko Mwigulu, na kumkaanga Mwigulu ni kuharibu mafuta kwa mtu asiyestahili. Mkaangeni anayempa maelekezo Mwigulu.
Nawasilisha kwenu Wakuu, naomba mjadala uwe wa staha.