SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Bado ni mapema sana kwa pande zote mbili kufanya maamuzi. Timu zote mbili za Simba na Yanga zimefanya usajili mzuri na zina vikosi vya kiushindani kwa mashindano ya ndani na nje.
Tuna nafasi ya kuwa na msimu mmoja mzuri sana wenye ushindani wa kweli ila hilo litatokea kama tutaweka silaha zote chini za nje ya uwanja. Hapa naongelea majungu, uzushi, propaganda za uongo, mapandikizi ya kuvuruga (mashabiki, wanachama, wachezaji na viongozi), rushwa, fitna na kurushiana majini na aina zingine za nguvu za giza dhidi ya wapinzani wako.
Chonde chonde mwanakwetu. Tuingie uwanjani tushindane, aliye bora ndiyo ashinde. Msimu huu tunahitaji kupata msimu wa kihistoria.
Kataa majungu, kataa habari za uzushi na uchochezi, kataa rushwa. Tukutane uwanjani, tucheze mpira.