Msimu wa 2019/2020 ligi kuu nchini Italia hatarini kuishia njiani

Msimu wa 2019/2020 ligi kuu nchini Italia hatarini kuishia njiani

Van Halen

Senior Member
Joined
Dec 4, 2013
Posts
116
Reaction score
191
Msimu wa 2019/2020 Ligi Kuu nchini Italia, maarufu kwa jina la Serie A, huenda ukakomea njiani, kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya CORONA, ambalo limeendelea kuitesa nchi hiyo.

Ligi hiyo ambayo kwa sasa imesimamishwa, inatarajiwa kuendelea mnamo April 3, mwaka huu, huku Rais wa shirikisho la soka nchini humo, Gabriele Gravina akisema kuwa, tayari wameshandaa mpango B, endapo ligi hiyo ikishindwa kuendelea, ikiwemo kucheza play off kwa ajili ya kumpata bingwa, pamoja na timu zitakazoshiriki michuano ya Ulaya msimu ujao, sambamba na kupata timu zitakazo shuka daraja.

Mpango mwengine ambao bado unajadiliwa, ni kumaliza ligi kwa msimamo wa sasa, ambapo kama itakubaliwa hivyo, Juventus watatawazwa mabingwa tena kwa msimu wa tisa mfululizo, kutokana na wao kuwa kileleni kwa sasa.

images%20(3).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom