Msimu wa kilimo cha vuli ndio huu, serikali punguza bei ya mbegu za mahindi

Msimu wa kilimo cha vuli ndio huu, serikali punguza bei ya mbegu za mahindi

Wakulima wachache wa vijijini watamudu bei ya shilingi 15 elfu kwa mfiuko wa kilo mbili! Hakuna, watatumia mbegu zao ambazo hazina tija na ni za muda mrefu kuweza kuvuna na mvua hizi fupi!

Soma Pia: Rais Samia aagiza mahindi kununuliwa kwa Tsh 700 kwa kilo
Mbegu gan hiyo? Kwa Msimu huu Dk imeanzia elfu 16 ya Tz.. ya Zambia elfu 20.. mambo ni 🔥 nadhani lengo lao tusilime kabisa.. kwa maana haiingii akilini bei kupanda kiasi hicho! Je, Msimu wenyewe ukifika bei itakuwaje?? Kama sasa ndivyo!
 
Naam hata zile Mbegu za ruzuku bei elekezi ni 14K Hadi 16K.Kazi IPO Mwaka huu.Na Kwa wafanyabiashara nimeona bei DKC na Lubango Kwa Geita Hadi 18K Kwa Mfuko wa 2KG.
 
Hii nchi Kilimo ni kigumu sana kwakweli.
Kulima ni ghalama kubwa, masoko ni haba. Mauzo ni bei ya chini.
 
Mbolea Mfuko mmoja wa 50kg ni 120,000.
Kilimo ni sekta inayotegemewa tz lakini vikwazo ni vingi na serikali Iko kimya
 
Mbegu gan hiyo? Kwa Msimu huu Dk imeanzia elfu 16 ya Tz.. ya Zambia elfu 20.. mambo ni 🔥 nadhani lengo lao tusilime kabisa.. kwa maana haiingii akilini bei kupanda kiasi hicho! Je, Msimu wenyewe ukifika bei itakuwaje?? Kama sasa ndivyo!
Vuli kwani si msimu rasmi wa kilimo?
 
Hii nchi Kilimo ni kigumu sana kwakweli.
Kulima ni ghalama kubwa, masoko ni haba. Mauzo ni bei ya chini.
Ni sahihi. Sisi nyanda za juu kusini tunapigika kweli ila kwa kuwa hatuna namna tutafanyaje.

Mwaka huu nimelima ekari 10 za mahindi ya Gobo. Nimetafuta mbegu ya Mahindi ya Gobo maarufu sana huku kwetu ya Kitale 628. Mzee wametuuzia mbegu fake, sijawahi kupata hasara kama mwaka huu.

Ukilalamika kwa hawa TOSCI, Utazungushwa hadi ukome. Imebidi tukubali tu kwani kuna Mbegu fake zinazalishwa pale Makambako na TOSCI wanafahamu.

Kilimo ni kazi sana. Pamoja na kupanda mbegu fake, anatokea Dalali naye anakuja kukutapeli hivyo hivyo.

Kama sijala kwa pressure msimu uliopita, sitakufa tena maana niliumia sana.
 
habari za asubuhi jamani ndugu wakulima wenzangu kuna fursa ya kuuza mashudu ya alizeti china tuchangamikie fursa
 
Back
Top Bottom