Msimu wa kilimo cha vuli ndio huu, serikali punguza bei ya mbegu za mahindi

Mbegu gan hiyo? Kwa Msimu huu Dk imeanzia elfu 16 ya Tz.. ya Zambia elfu 20.. mambo ni 🔥 nadhani lengo lao tusilime kabisa.. kwa maana haiingii akilini bei kupanda kiasi hicho! Je, Msimu wenyewe ukifika bei itakuwaje?? Kama sasa ndivyo!
 
Naam hata zile Mbegu za ruzuku bei elekezi ni 14K Hadi 16K.Kazi IPO Mwaka huu.Na Kwa wafanyabiashara nimeona bei DKC na Lubango Kwa Geita Hadi 18K Kwa Mfuko wa 2KG.
 
Hii nchi Kilimo ni kigumu sana kwakweli.
Kulima ni ghalama kubwa, masoko ni haba. Mauzo ni bei ya chini.
 
Mbolea Mfuko mmoja wa 50kg ni 120,000.
Kilimo ni sekta inayotegemewa tz lakini vikwazo ni vingi na serikali Iko kimya
 
Mbegu gan hiyo? Kwa Msimu huu Dk imeanzia elfu 16 ya Tz.. ya Zambia elfu 20.. mambo ni 🔥 nadhani lengo lao tusilime kabisa.. kwa maana haiingii akilini bei kupanda kiasi hicho! Je, Msimu wenyewe ukifika bei itakuwaje?? Kama sasa ndivyo!
Vuli kwani si msimu rasmi wa kilimo?
 
Hii nchi Kilimo ni kigumu sana kwakweli.
Kulima ni ghalama kubwa, masoko ni haba. Mauzo ni bei ya chini.
Ni sahihi. Sisi nyanda za juu kusini tunapigika kweli ila kwa kuwa hatuna namna tutafanyaje.

Mwaka huu nimelima ekari 10 za mahindi ya Gobo. Nimetafuta mbegu ya Mahindi ya Gobo maarufu sana huku kwetu ya Kitale 628. Mzee wametuuzia mbegu fake, sijawahi kupata hasara kama mwaka huu.

Ukilalamika kwa hawa TOSCI, Utazungushwa hadi ukome. Imebidi tukubali tu kwani kuna Mbegu fake zinazalishwa pale Makambako na TOSCI wanafahamu.

Kilimo ni kazi sana. Pamoja na kupanda mbegu fake, anatokea Dalali naye anakuja kukutapeli hivyo hivyo.

Kama sijala kwa pressure msimu uliopita, sitakufa tena maana niliumia sana.
 
habari za asubuhi jamani ndugu wakulima wenzangu kuna fursa ya kuuza mashudu ya alizeti china tuchangamikie fursa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…