Msingi mkubwa wa makanisa ya kilokole ya zamani ni kujitenga na uzinzi na ulevi. Sasa hivi msingi mkubwa ni kutoa sadaka

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!
Nilitaka kuandika kitabu muda kidogo chenye title inayosema "Kanisa la uzinzi" ila nimekosa muda kidogo, ila ipo siku nitaandika hichi kitabu ili angalau watu wachache wapone.
Kanisa la sasa limepatikana, silaha ya mwisho ya Ibilisi ambayo ni roho ya uzinzi inafanya kazi kwa kasi sana.
Uzinzi hauangalii jinsi unavyonena kwa lugha au jinsi unavyotoa pepo wachafu kwa watu wengine.
Uzinzi una njia mbili tu za kuukwepa.
1. Kuukimbia
2. Kukataa (kuukemea)
Hii njia namba 2 inaanza kwa kiongozi kisha muumini binafsi aukatae na kuukemea.
Wachungaji hawana ujasiri wa kukemea uzinzi kwakuwa nao wana vifungo vya uzinzi.
Ukimwona mchungaji wako anahubiri mara 5 na hagusii hili janga la uzinzi jua tu naye yuko kifungoni na hajui anatokaje.
Zamani ukizini tu lazima mzee wa kanisa au mchungaji atajua na atakuita akuambie asemayo Mungu ila sasa kanisa liko na giza totolo, halioni tena.
Labda sadaka tu ndizo zinaonekana kwa macho ya rohoni na mwilini maana ndio msingi mkubwa wa makanisa ya sasa .
 
Tatizo la walokole wengi liko sehemu moja tu; kwao wakizini wao kwa wao, huchukulia kama siyo dhambi vile! Na kiukweli hawa watu wanatafunana kweli wenyewe kwa wenyewe!

Ila ikatokea mlokole sasa akachukuliwa na Mkatoliki au Muislam, basi hapo ndiyo huchukulia ni dhambi kubwa! Na mapepo yatakemewa usiku kucha.
 
Hapana.
Uzinzi kwa walokole ni mwiko iwe nyumbani au ugenini
 
Tatizo la walokole wengi liko sehemu moja tu; kwao wakizini wao kwa wao, huchukulia kama siyo dhambi vile! Na kiukweli hawa watu wanatafunana kweli wenyewe kwa wenyewe!

Ila ikatokea mlokole sasa akachukuliwa na Mkatoliki au Muislam, basi hapo ndiyo huchukulia ni dhambi kubwa! Na mapepo yatakemewa usiku kucha.
Kuzini ni dhambi inayoliteketeza kanisa la kilokole. Hakuna mchungaji asiye na nyumba ndogo. Wajane wengi au wanawake waliotalikiwa walipo huko wanachukuliwa na walokole wenye uwezo. Kingine ni utapeli. Ndani ya kanisa la walokole kuna utapeli mkubwa sana. Uchu wa fedha na mali hausemekani.
 
Hatari
 
Wanasemaga wameanguka kiroho 😃
 
Kuzini ni dhambi inayoliteketeza kanisa la kilokole. Hakuna mchungaji asiye na nyumba ndogo. Wajane wengi au wanawake waliotalikiwa walipo huko wanachukuliwa na walokole wenye uwezo. Kingine ni utapeli. Ndani ya kanisa la walokole kuna utapeli mkubwa sana. Uchu wa fedha na mali hausemekani.
Wachungaji wa haya makanisa kuna wakati hudai fungu la 10 kwa nguvu aisee! Na hapo bado hujaongelea kale ka ubaguzi ka walio nacho, na wale wenzangu na mimi wasio nacho!
Unakuta Mchungaji/Nabii/Mtume anawagawanya wana kondoo wake katika makundi tofauti tofauti kwa misingi ya kipato!

Kwa kweli hawa ndugu zetu na wenyewe wanatakiwa kujitathmini! Wanatupiga sana mawe sisi Wakatoliki, huku na wenyewe wakiwa na madhambi yao chungu nzima.
 
Wale wa zamani wa ukweli, walikuwa wanaomba kwa kulia ,utakuta macho yamewavimba, ila siku hizi ni akina bongo movies, kwa sababa wame test zari za maigizo Mungu amewaacha ndio wanaendeleza Gospel commedy, wapo wengi walianzia maigizo ya kawaida walivyochungulia fursa wakaenda hapo makumira shuta kuchukua ka certificate, wakanunua wakaingia mitaani kuanza kukusanya sadaka za wajinga baada ya shuhuda feki. Wapo kama yule wa Arusha anayetengeneza kiki za kizamani kwa kuwatumia bongo movies, kuwapa fedha na magari
 
Wachungaji wa haya makanisa kuna wakati hudai fungu la 10 kwa nguvu aisee! Na hapo bado hujaongelea kale ka ubaguzi ka walio nacho, na wale wenzangu na mimi wasio nacho!
Unakuta Mchungaji/Nabii/Mtume anawagawanya wana kondoo wake katika makundi tofauti tofauti kwa misingi ya kipato!

Kwa kweli hawa ndugu zetu na wenyewe wanatakiwa kujitathmini! Wanatupiga sana mawe sisi Wakatoliki, huku na wenyewe wakiwa na madhambi yao chungu nzima.
Ni muda tu makanisa ya walokole yatapotea kwenye ramani. Trust me. Wanajimaliza wenyewe. Injili ya walokole ya siku hizi imelenga kwenye kutatua matatizo ya kibinadamu na siyo kuishi maisha ya kumcha Mungu. Tatizo linakuja wanapo-fake kuwa kuna watu wamatatuliwa matatizo yao. Kuna ule msemo kuwa uongo huchukuwa lift kuapnda ngazi lakini ukweli hutumia ngazi kukwea...
 
Ndomana huyu mwamba kwake kapiga maarufuku ujinga huu
Kwanza inaongezea tu kufanya watu wawe mazuzu na mandondocha

Ova
Screenshot_20221004-172151_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom