Msingi wa biashara ni wateja sio mtaji

Msingi wa biashara ni wateja sio mtaji

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Biashara nyingi sana hufa,sio kwa kukosa mtaji bali ni kwa kukosa wateja

Ukifuatilia kwa karibu hutasikia kwamba kuna biashara eti ili kufa kwa sababu ilikosa mtaji,nyingi hufa kwa kukosa wateja.hata zile ambazo huwa na ufinyu wa mtaji bado ukifuatilia kwa ndani utakosa root cause ni kukosa wateja.

Kwa maana nyingine basi uwezo wa kumridhisha mteja na moja kati ya jambo muhimu sana katika biashara.La muhimu zaidi ni kumfahamu mteja wake vizuri.Wengi huanza biashara bila kuwekeza katika kuwafahamu wateja wao.Hufikiri kwamba ukishakuwa na bidhaa/huduma basi utapata wateja kumbe sivyo.

Ukweli ni kwamba kabla ya kuanza biashara lazima uwafahamu wateja wako na hata baada ya kuanza biashara lazima uwe na taarifa za wateja wao.Hata kwenye maduka ya rejareaja huko mtaani,wauzaji wanatambua hilo.Huwa na kumbukumbu kuhusu wateja wao hata kama sio za kuandika lakini huwa wanajua wateja wanaishi mazingira gani,hununua bidhaa gani zaidi,huwa na kipato gani na kama wana kazi au hawana.Taarifa hizi huwasaidia sana katika kufanya maamuzi ya kibiashara pasi na wao kujua kwamba wanatumia mbinu kubwa sana katika kuendesha biashara zao.

Kutokana na mamendeleo ya teknolojia sasa inawezekana kabisa kufuatilia kwa ukaribu taarifa za wateja wako kwa kutumia mifumo ya kisasa na kuhakikisha unazo taarifa za wateja wako,kipato chao manunuzi yao na taarifa zao za muhimu ambazo zinakuwezesha kufanya maamuzi ya kibiashara.

Mifumo hii inaitwa CRM-Customer relations Systems.

Mifumo hii imetengenezwa mahususi kwa ajili ya kukuwezesha wewe kukusanya taarifa za wateja wako na kufanya maamuzi kwa kutegemea hali zao kwa wakati husika

Tunatoa huduma za kukusanya taarifa za wateja wako na kuzihifadhi katika mfumo wa CRM pamoja na kukupatia ripoti mbalimbali zitakazokuwezesha kufanya maamuzi ya kibiashara.Pia tutakufundisha namna bora ya kutumia taarifa zako katika kufanya maamuzi kwa kutumia mifumo na kuisimamia biashara yako kwa kutumia mifumo ya CRM.

Kwa msaada na maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia email:masokotz@yahoo.com

Karibu sana
 
Back
Top Bottom