SoC04 Msingi wa mapinduzi ya teknologia na sayansi kwa maendeleo ya viwanda nchini

SoC04 Msingi wa mapinduzi ya teknologia na sayansi kwa maendeleo ya viwanda nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

fundamental secret

New Member
Joined
Jun 11, 2024
Posts
4
Reaction score
3
Nchi yetu Tanzania na bara lote la Afrika linapaswa kuanza na mambo yafuatayo ili kuleta mapinduzi ya viwanda. Kwanza, ni muhimu kuunda sera zitakazo ongeza uwezo wa watu wabunifu kujiamini katika kazi zao. Pili, ni kubadili fikra za jamii juu ya uwezo wa wazalendo wenye vipaji mbalimbali vya kuunda; serikali pia inapaswa kuwaamini kwa vitendo kuwa wanaweza. Kisha, serikali iandae orodha ya bidhaa zote za kila aina zinazotumika nchini. Baada ya hapo, serikali ifanye uchunguzi wa aina zote za bidhaa na uwezo wetu wa mwanzo tunazoweza kutengeneza wenyewe.

Kisha, itathmini uwezo wetu wa kuzalisha bidhaa hizo. Zile tunazoweza kuzalisha kwa kukidhi soko, tutafunga soko la nje na kuleta ndani zile tunazoshindwa kuzalisha kwa wingi wa kutosha. Kwa zile bidhaa tunazoweza kujitosheleza, tutapunguza idadi ya kuagiza kutoka nje. Kisha, itatengenezwa sheria yenye meno kuzibiti uagizaji wa bidhaa tunazoweza kujitosheleza.

Baada ya hapo, serikali inapaswa kuunda vituo maalum vya watu wenye vipaji na kuwawezesha kwa mahitaji yao muhimu kwa maendeleo ya bunifu zao. Pia, kuwakutanisha na watu wenye mitaji ya kuwekeza kwenye kazi zao, wa ndani na nje. Serikali itatunga sheria juu ya uwekezaji kwenye maendeleo ya teknolojia nchini na kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya kutengenezea na kukuza teknolojia kwa wataalamu.

Serikali itaanzisha mkakati wa kitaifa wenye malengo maalum ya kuwapeleka nje watu wenye vipaji kwa kazi maalum ya kujifunza na kuchunguza teknolojia mbalimbali duniani. Serikali itaandaa mpango maalum wa kuongeza kwenye orodha kila aina ya bidhaa tunazofanikiwa kutengeneza ndani na kuondoa kabisa au kupunguza kwenye orodha ya manunuzi kutoka nje.

Serikali itaajiri wataalamu maalum kutoka nje kuja ndani kushirikiana na wataalamu wa ndani. Mwisho, chama tawala kitaingia mkataba wa kitaifa na nchi pamoja na vyama vyote vya siasa katika mkakati huu muhimu kwa madhumuni ya kuulinda usiasiliwe na siasa pamoja na mabadiliko ya watawala mpaka lengo litimie.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom