Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Habari za wakti huu,
Ni matumaini yangu kwamba nyote mnaendelea Vizuri na Shughuli za Ujenzi wa Taifa. Hata mimi niko Salama.
Ni muda mrefu sana tangu niweke andiko rasmi hapa Jukwaani, hata hivyo nimekuwa nikiendelee kushirikiana na wadau katika kutafuta suluhu na fursa za kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo tunakutana nazo.Leo nataka nilete mjadala mfupi lakini wa kipekee sana ambao unaweza kubadili kabisa aina ya maisha unayoishi. Mjadala wenyewe Unahusu UTAJIRI.
Utajiri ni nini? Kwa wengine utajiri ni kuwa na mali nyingi zenye thamni kubwa,kwa wengine utajiri na kuwa na PESA,kwa wengine utajiri ni kuwa na biashara zenye mzunguko mkubwa wa PESA na kwa wengine utajiri ni kuwa na uhakika wa kipato.Vile vule Utajiri ni kuwa na maisha ya furaha, amani, utulivu, kuwa na afya na siha na mwili na kuweza kupata mahitaji yako ya msingi kwa wakti unaoyahitaji.
Kwa mtazamo wangu mimi, Utajiri ni kuwa na hivyo vyote nilivyotaja na kuwa na uwezo na uhakika wa kuvipata katika Maisha yako ya mbeleni hata katika kizazi cha tatu na cha nne.Kwa Mtazamo wangu huu Utajiri ni MFUMO wa maisha.Hivyo basi ninapoandika kuhusu Msingi wa Utajiri katika KARNE ya 21 naomba sana uzingatie kwamba ninazungumzia zaidi msingi wa KIMFUMO.Mfumo huu ninauona kwa watu ambao wanaonekana kuwa nia maskini na wanaoonekana kuwa ni Matajiri na hivyo basi nitaweka hapa Misingi hiyo ili tuijadili kwa Pamoja:
Nawatakieni kila la heri katika shughuli zenu.

- Msingi wa kwanza ni Kuchukua hatua(Taking Action):Ili uingie katika mfumo wa Utajiri ni lazima uwe na Desturi na kawaida ya kuchukua hatua na kufanya/kutenda jambo.Usiwe na hofu ya kukosea/kupoteza bali uwe na hamu ya kuchukua hatua,kujifunza na kukua huku ukiboresha.
- Msingi wa Pili wa kuingia katika Mfumo wa Utajiri ni Kujipanga/Kupanga: Wanasema kupanga ni kuchagua na kwa mtu anayetaka kuwa Tajiri Ukweli wa kauli hii ni mkubwa sana.Kumbuka kwamba Huwezi wewe kufanya kila kitu au kuwa kila kitu au kuwa kila mahali.Kuna wakti itakubidi Uchague.Hivyo Basi Hakikisha unajipanga vizuri katika kila Jamba unalofanya.
- Msingi wa Tatu ni kutumia Nguvu ya Mtandao(Power of Networks): Fahamu kwamba huku Duniani katika kila watu 6 unaowafahamu wote wanawafamua watu 6 wengine ambao na wewe unawafahamu na ambao nao wanawafahamu watu 6 ambao na wewe unawafahamu mpaka mtu wa sita.Kwa lugha nyingine kuna watu 6*6*6*6*6*6*6 ambao wewe unawafahmu moja kwa moja au kwa kupitia watu unaowafamu so JITAHIDI katika mzungu wako uwe na watu SITA ambao wanaendana na Ndoto na maono yako na wao watakupeleka kwa watu wengine wote katika mtandao wako.Tumia akili kutengeneza na kutumia Mtandao wako vizuri.
- Msingi wa nne ni Nidhamu(Power of Discipline):Hili sihitaji kusema sana.Kila mtu ambaye unamuona hajafanikikwa katika Jambo lolote ambalo amelifanya ukifuatilia Chanzo Utakuta Alikosa au kupungukiwa na Nidhamu.na Pia kila mtu ambaye alifanikiwa katika jambo lolote utaona kwamba alikuwa na kiango cha Nidhamu.Nidhamu ya muda,Nidhamu ya Pesa,Nidhamu ya kujifunza,nidhamu ya kazi,nidhamu ya kula,nidhamu ya kupumzika,nidhamu ya kucheza,nidhamu ya kuimba,nidhamu ya kusali n.k.Nidhamu inaleta ORDER na ORDER ni mafanikio
- Msingi wa Tano ni kujijengea UWEZO wa kutumia FURSA(Dunia haina uhaba wa FURSA) Fursa zipo nyingi sana ili sio kila fursa mtu unaweza kuitumia.Hivyo basi ili kuingia katika mfumo wa utajiri ni lazima ujijengee uwezo wa kutumi Fursa.Hili unaweza kufanya kwa kujifunza,kutumia PESA ikufanyie kazi,kutafuta aina ya watu ambao wanauwezo zaidi yako.Zote hizo zitakupa uwezo wa kutumia FURSA mbalimbali kwa ukamilifu.
Nawatakieni kila la heri katika shughuli zenu.