Msiolipa kodi stahiki hamna uhalali wa kutuwekea Tozo juu ya kodi tunazolipa

Msiolipa kodi stahiki hamna uhalali wa kutuwekea Tozo juu ya kodi tunazolipa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Viongozi wetu hawana nia ya kulipa kodi kama inavyostahili. Ili kukwepa kulipa stahiki yao kamili ya kodi, sehemu kubwa zaidi ya mapato yao wameiita "posho."

Kwenye orodha ya wakwepa kodi hao yumu Mwigulu na timu nzima ya vigogo wote. Almaarufu walamba asali.

Kwa wenzetu kunaponoga:

IMG_20220913_112652_836.jpg


Enyi huko serikalini, bungeni, nk hamuoni hata aibu wandugu?

Ewe Mwigulu, Majaliwa, Samia na wenzenu kulikoni kuwatwisha wananchi mzigo wa tozo hali nyie kodi za msingi tu haziwahusu?

Au ninyi masikio yenu ni Ile hadi uvumilivu utushinde?

Lipeni kodi haipo haja ya tozo wala timu ya kuzichunguza.
 
Wewe

KWA katiba yetu wanasiasa hawalipi kodi !unajua hilo!!?

Mbunge hakatwi kodi kwenye mshahara!? Hata Rais hivo hivo!!?

Wenye hekima Wanaimba HIVI;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
 
Wewe

KWA katiba yetu wanasiasa hawalipi kodi !unajua hilo!!?

Mbunge hakatwi kodi kwenye mshahara!? Hata Rais hivo hivo!!?

Wenye hekima Wanaimba HIVI;-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"

Janja janja,mishahara wanaita posho. Posho na marupurupu kibao hawalipi kodi kama mapato yao.

Aibu kwao wote wanaotuletea sisi tozo zaidi.

Naunga mkono hoja, katiba mpya ni sasa.
 
Kwanza mishahara ya wabunge na kiinua mgongo viondolewe kabisa ubunge iwe kazi ya kujitolea serikali itawagharamia kile kipindi cha mikutano tu mikutano ikiisha wabunge wanarudi kuendelea na shughuli zao za kuwaingizia kipato, ni ujinga kumlipa mshahara mbunge kila mwezi wakati muda wanaokaa bungeni kwa kwa mwaka hata miezi mitatu haiishi.
 
Wanao jifanya wazalendo no 1 hawalipi Kodi alafu kutwa kusisitiza wananchi walipe Kodi Kama ishara ya uzalendo alafu mwisho wazalendo no 1 wanatumia Kodi kujilipa posho na kununua v8.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wanao jifanya wazalendo no 1 hawalipi Kodi alafu kutwa kusisitiza wananchi walipe Kodi Kama ishara ya uzalendo alafu mwisho wazalendo no 1 wanatumia Kodi kujilipa posho na kununua v8

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Kama vile haitoshi wanatusokomeza na tozo juu. Wapi maofisini kujinufaisha wenyewe na familia zao.
 
Back
Top Bottom