Msipo sema hakuna wa kuwasemea, ulizeni nje ya kujenga madarasa kwa pesa ya mkopo wa Covid19 Nini kingine?

Msipo sema hakuna wa kuwasemea, ulizeni nje ya kujenga madarasa kwa pesa ya mkopo wa Covid19 Nini kingine?

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Tusizuiliwe kuhoji, pesa za kuendelea miradi mathalani bwawa la Nyerere, ujenzi wa reli na miradi mingine Raisi Mwendazake aliwai kusema sio mara moja au mara mbili, kuwa pesa zipooooooo!nasema pesa zipoooo in his voice like akitamka nileteeni "Gwajima,nasema nileteeni Gwajima Nileteeni Gwajima"

Lazima tuhoji mwaka mmoja wa Magufuli Nini kilifanyika ndani ya mwaka mmoja na tuseme ukweli ndani ya mwaka mmoja wa Rais aliyepomadarakani Nini kafanya nje ya ujenzi wa shule za mikopo?

Najua ntaambiwa amefungua nchi, hivi nchi ilifungwa alafu ikawa inakopeshekaje?mbona hakwenda nje kama mama yetu na alikopeshekaje?

Lazima najua mtaniambia,fursa zimefunguka?zipi hizo?

Mtaniambia amrudisha nidhamu kazini eti kisa sabaya yupo jera?

Semeni vinavyo onekana Rais amefanya Nini hacheni makala zinazoandaliwa na mawaziri za uongo uongo,

Twambieni mtaniambia amefungulia uhuru wa habari kivipi? Mswada gani umepelekwa bungeni kubadili Sheri mbovu zinazosimamia habar Tanzania?

Niambieni hivi mnajua pembejeo zimepanda bei,hivi mnajua vifaa vya ujenzi vinapanda Kila siku?

Hivi mnajua hakuna salary increament to civil servant?

Onesheni kwa macho tuone na tuguse sisi wengine ni wakina Tomaso mpka tuone na kugusa ndo tunaamini vinginevyo tuache cheap politics tumezichoka.
 
Ngoja waje wapiga makofi na sifia sifia utajua hujui! Waziri anasimama anaongea ujinga ili asikike anamuunga mkono mama!
 
Nje na madarasa ya mkopo wa kovidi..naona wanapuyanga tu.

Anyway jiandae kuwajibu chawa wa mama..waliomwagwa jf kuja kueneza propaganda kwa vipande vya pesa.

#MaendeleoHayanaChama
 
jera
hacheni

Huyu sijui kabila gani vile!!!
Tusizuiliwe kuhoji, pesa za kuendelea miradi mathalani bwawa la Nyerere, ujenzi wa reli na miradi mingine Raisi Mwendazake aliwai kusema sio mara moja au mara mbili, kuwa pesa zipooooooo!nasema pesa zipoooo in his voice like akitamka nileteeni "Gwajima,nasema nileteeni Gwajima Nileteeni Gwajima"...
 
Tusizuiliwe kuhoji, pesa za kuendelea miradi mathalani bwawa la Nyerere, ujenzi wa reli na miradi mingine Raisi Mwendazake aliwai kusema sio mara moja au mara mbili, kuwa pesa zipooooooo!nasema pesa zipoooo in his voice like akitamka nileteeni "Gwajima,nasema nileteeni Gwajima Nileteeni Gwajima"...

Magufuli aliacha pesa za kulipia bwawa na treni? Ziko wapi? Mikopo yote Magufuli aliyochukuwa unafikiri nani analipa?.

Kilubwa ni ongezeko la uwekezaji na huu matokeo yake yatakuwa kukuza uchumi, pato la taifa na miradi itaanza kuongezeka. Huwezi kuongeza tu matumizi bila kuongeza kipato na kipato ni kuongeza uwekezaji.

Hii ndiyo maana serikali inahimiza uwekezaji sana sijui kama unaelewa faida ya uwekezaji. Uwekezaji huwezi kuona matunda kwa mwaka mmoja! Jiulize tu Nyumba ya kawaida inachukuwa muda gani kujenga!
 
Nje na madarasa ya mkopo wa kovidi..naona wanapuyanga tu.

Anyway jiandae kuwajibu chawa wa mama..waliomwagwa jf kuja kueneza propaganda kwa vipande vya pesa.

#MaendeleoHayanaChama
Mkopo wa kovidi
1. Kujenga madarasa
2. Ujenzi vyuo vya veta 25 wilaya na 4 mikoa
3. Ujenzi wa ICU na EMD
4. Ununuzi wa mitambo CT SCAN, MRI n.k
5. Ununuzi wa ambulance 195
6. Miradi ya maji 218 mijini na vijijini
7. Ujenzi wa mabweni 50 kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu
8. Uboreshaji miundombinu kwenye hifadhi zetu

Hayo ni kwa uchache ...

Nje ya pesa ya uviko

1. Ujenzi wa vituo vya afya
2. Ujenzi wa zahanati
3. Ujenzi wa shule za kata 214 kati ya 1000
4. Ujenzi wa barabara tarura, kila jimbo 1.5 billion
5. Ujenzi wa hospitali za halmashauri 28

Kwa uchache, nutakuletea ripoti nzima kutoka tamisemi
 
Mkopo wa kovidi
1. Kujenga madarasa
2. Ujenzi vyuo vya veta 25 wilaya na 4 mikoa...
Mwamba yawezekana unahoja na nakubaliana na wewe tafadhali naomba PC za Kila uliro lisema Ili niamini maana Mimi ni tomaso
 
Mwamba yawezekana unahoja na nakubaliana na wewe tafadhali naomba PC za Kila uliro lisema Ili niamini maana Mimi ni tomaso
1. Ujenzi wa maeneo ya biashara kwenye majiji na miji maarufu machinga

2. Ujenzi wa kituo cha uviko Kasulu Kigoma

3. Wameajiriwa Watumishi kada ya afya kwa mikataba ya miezi sita kwenye halmashauri zote

4. Ujenzi wa shule shikizi hizi ni shule za msingi kwenye maeneo yale ambayo watoto wanasomea kwenye miti au vibanda umiza halmashauri zote

Alooo ni vingi sana big up sana
 
Back
Top Bottom