Pre GE2025 Msipoleta Katiba Mpya, mtatuletea Utawala wa Jeshi huko mbele

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Tatizo la viongozi wengi ni kulewa madaraka bila kusoma nyakati. Msije hata siku mmoja kujidanganya kwamba Watanzania watabaki hivi hivi miaka hii ya mitandao.

Serikali isikojirudi na kutengeneza idara imara za kidemokrasia itatoa mwanya huko mbele kama zile nchi tunazoona wananchi wameona bora jeshi kuliko wanasiasa. Hivyo nashauri kutoka moyoni kabisa bila kuwa na chama kuweka katiba nzuri yenye usawa ni muhimu sana kama mnaona mbele. Msikofanya hivyo mtatuletea utawala wa kijeshi na kuchokwa.
 
Hilo jeshi nililitoa maanani siku Magufuli alipopokea makada walihamia ccm kuunga juhudi huko Arusha kwenye kamisheni ya jeshi, huku jeshi likiwa limetengwa kikatiba na siasa. Cha ajabu na CDF alikuwepo anatabasamu kuwa chama chao kinaimarika!
 
Hili angalizo nimelielewa sana. Hongera kwa kuona mbali.
 
Tunakoelekea, na mabadiliko yanayotokea duniani, hilo haliepukiki.

Tusubiri tuone matokeo ya mwisho ya SMO ya Russia huko Ukraine.
 
Ccm wanaamini Katiba haina umuhimu
 
Kwa sasa hawawezi kukuelewa. Hata Ghadafi hakuwa kuelewa lakini jeshi lile lile lililomlinda lilimtoa balu.
 
Wanasiasa wanaliamini jeshi lipo upande wao,
Siku watashangaa wamba hao wapo ikulu.
 
Ninachokiona ni CCM kutengeneza mazingira ya kutokea vurugu za kisiasa huko tuendako. CCM wamedhamiria kubaki madarakani kwa mabavu ya vyombo vya dola,wanaiba kura,wanachakachua kura kwa msaada wa polisi na TISS. Kwa kizazi chetu hiki bado maumivu ya utawala dhalimu wa CCM hayajakolea ndiyo maana utakuta hata baadhi ya wasomi wanasapoti udhalimu huu.

Lakini saa yaja ambayo maumivu haya yatafika kwenye mfuma na kizazi kijacho kitakuwa na ujasiri kuliko sisi tuliopo sasa ndipo watalianzisha bila kukoma,watawala watatumia majeshi kudhibiti vuguvugu hilo lakini kwa vile watu watakuwa wamepigika sana na kukata tamaa hawataigopa tena risasi na mabomu. Ikifika hapo majeshi nayo kwani na wenyewe ni watanzania hawatakubaali kuua watu wanaodai haki yao kwa kulinda kikundi kidogo cha watawala, ndipo watakuwa upande wa wananchi na ndiyo itakuwa mwisho wa CCM.

CCM imechagua kuingiza nchi kwenye umwagaji damu na kuondoka madarakani kwa fedheha. CCM wanalo chaguo nalo ni kuleta Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi na kuheshimu matakwa ya wananchi kupitia sanduku la kura. Huu ubabe wanaotangaza kila siku kuwa watatawala milele tayari hilo ni tangazo la machafuko ya kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…