#COVID19 Msisitizo wa kutumia vitakasa mikono kama ilivyokuwa wimbi la kwanza urudiwe

#COVID19 Msisitizo wa kutumia vitakasa mikono kama ilivyokuwa wimbi la kwanza urudiwe

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Mbona iliwezekana mwaka jana karibu kila duka na kila nyumba ilikuwa hukosi sanitizer nje nadhani ilisaidia sana mwamko ule wa kunawa ungeendelea Basi ingependeza sana.

Kwanza hata watoto wetu wanaozaliwa wangekuta tuna utamaduni wa kunawa. Ndugu zangu mikono inashika uchafu mwingi sana. ukijaribu kunawa na sanitizer utaona uchafu ukitoka na kufanya mikono kuwa salama zaidi.

Naomba nitoe rai kwa wizara ya afya iangalie ni namna gani watakuja na kampeni ya kuhamasisha kila duka au ofisi iwe na ndoo ya maji tiririka pamoja na sanitizer kwa kufanya hivyo tutakuwa tumejikinga na corona pamoja na magonjwa mengineyo.

Kwa kuwa viongozi wa Serikali hii wengi wamepoteza mvuto mbele ya wananchi basi yafaa watumiwe watu wenye ushawishi ili wahamasishe watu kama vile Bakheresa, Asha-Rose Migiro, wasanii wa comed kina mtanga sijui masele, joti n.k (Wale ambao hawakuitwa kwenye makampeni ya uchaguzi mkuu hivyo bado hawana mgawanyo wa mashabiki).

Kuendelea kutumia viongozi hawahawa tulionao kina Dorothy, kina Makalla hakutasaidia kwa vile watu wamewadharau kidogo ndo maana matamko yao hayazingatiwi.
 
Kama kila wakati wenye malengo ovu Kwa taifa wanaimba, tusiende kuchanjwa,hako ni kakorona tu hakatutishi, kwa bure elimu ya kitanzania, hapa tunahitaji kutafuta mchawi ni nani? Kichaka kinacho tumiwa na wasiokuwa na nia njema kwa taifa, ni kamsemo kuwa chanjo ni hiari na sii lazima.
 
Watu hawajawadharau kina Dorothy tu, wamezarau hata wanasayansi wetu wote kwenye hili suala la chanjo.

Mwanasayansi alisema mwezi Februari chanjo hazima maana, hazijathibitishwa, zimetolewa kwa dharula, zina madhara. Halafu mtu huyo huyo mwezi May ama June anasema chanjo nzuri, zinasaidia, zinaokoa, zinazuia, utamuelewaje?

Mfano, Juzi India iliruhusu chanjo ya J&J kama tuliyoletewa hapa itumike kwa dharula tu, pale hakuna chanjo nyingine ndio J&J itumike. Na hii wameifanya baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa muda mrefu. Sis chanjo imekuja leo, kesho wanasayansi wetu wanasema iko salama, wameichunguza lini?

Mwisho na cha ajabu kabisa, form ya kupata chanjo inaiongelea WHO kwenye kila kitu, kwani chanjo tumeletewa na WHO ama wizara ya afya ya Tanzania?
 
Mwaka jana tulikuwa vizuri sana kipindi cha mwanzo, ila baada ya kupima mapapai na mbuzi kukutwa na corona na yule dada wa maabara nimemsahau jina kutumbuliwa.

Watanzania hawajawahi kuchukulia corona serious tena mpaka leo hii.
 
Mwaka jana tulikuwa vizuri sana kipindi cha mwanzo, ila baada ya kupima mapapai na mbuzi kukutwa na corona na yule dada wa maabara nimemsahau jina kutumbuliwa.

Watanzania hawajawahi kuchukulia corona serious tena mpaka leo hii.
Hapa inafaa watu watambue umuhimu wa matumizi bora ya akili na mdomo.
 
Polepole kasema tutoe hofu ndio silaha muhimu kuishinda corona na kufanya uchumi wetu ukue kama mwaka jana!
 
Nguvu kubwa imehamishiwa kwenye chanjo kwa sasa. Hata upimaji sio kipaumbele tena. Tabia ya kuchukua tahadhari kwa kunawa na kutumia vitakasa mikono ilitakiwa iwe endelevu, inamanufaa mengi ukiachilia mbali janga la uviko 19.
 
Watu hawajawadharau kina Dorothy tu, wamezarau hata wanasayansi wetu wote kwenye hili suala la chanjo.

Mwanasayansi alisema mwezi Februari chanjo hazima maana, hazijathibitishwa, zimetolewa kwa dharula, zina madhara. Halafu mtu huyo huyo mwezi May ama June anasema chanjo nzuri, zinasaidia, zinaokoa, zinazuia, utamuelewaje?....
Haohao India walitengeneza chanjo yao baada ya kuona imefeli ndio wamerudi kwenye Jenssen. Sisi na India nani wanajua zaidi?
 
Back
Top Bottom