Msitu Wa Kuabudia Wa Iganjo

Msitu Wa Kuabudia Wa Iganjo

Uyole CTE

Member
Joined
Apr 17, 2015
Posts
7
Reaction score
12
Msitu huu wa kimila (asili) wa iganjo unapatikana Uyole igawilo Mkoani Mbeya, ni moja kati ya misitu yenye uoto wa asili katika mkoa wa Mbeya, hapo awali msitu huu ulikuwa mkubwa sana kutokana na shughuri za binadamu zinazoendelea kama kilimo na ujenzi umepungua kiasi, msitu huu umezungukwa na mashamba yanayotumika na wakazi kwa kilimos, kuna aina mbalimbali za miti na mimea ya asili katika msitu huu, Ni mahali ambapo hutumiwa na kabila la wasafwa katika sherehe za matambiko pamoja na ibada zao za kimila.

Sherehe za kimila hufanyika mwezi wa nane kila baada ya miaka miwili na inahusisha vitu vifuatavyo:-

· kuwakumbuka na kuwaombe ndugu, jamaa na marafiki waliokufa

· Kufanya matambiko kama vile kuombea Nchi na dunia kwa ujumla, Mvua, Amani, magojwa, biashara na mambo mengine mbalimbali yanayotuzunguka.

· Sherehe hizi zinahusisha wasafwa wote na wageni waalikwa kufurahi kwa pamoja bila kujali dini, kabila wala itikadi.

Sherehe hizi za kimila huongozwa na Chifu (mwene) wa kisafwa anaeongoza sasa anaetambulika kwa jina la Mwene Rocketi Mwanshinga ambaye ndio chifu mkuu wa kabila la wasafwa wote Mbeya na Tanzania kwa ujumla, mwene mkuu hawi peke yake katika matambiko haya ya kimila huambatana na ma mwene wengine wa maeneo yake.

Msitu huo unalindwa kijadi na unamaajabu mengi sana kuna, zipo taratibu mbalimbali za kufuata ili kuweza kungia katika msitu, moja wapo ni kutoa taarifa kwa kiongozi wa jadi ili kupewa kibali cha kuingia na endapo ukakaidi kwa maelezo ya mwene utajikuta unazunguka ndani yam situ pasipo kufanikiwa kuona njia ya kutokea, pia kuna sehemu ambazo huruhusiwi kupiga picha, siku ya matambiko huruhusiwi kuvaa nguo zenye rangi nyekundu N.K..

Karibu sana uyole cultural tourism enterprise
 
Back
Top Bottom