Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Nchini Romania, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo, jirani na mpaka wa nchi ya German ndiko hupatikana msitu wa wauzauza wa Hoia-Baciu.
Tukiachana na msitu wa mauzauza wa Njombe tuliouzoea, msitu wa mauzauza wa Hoia-Baciu ni noma, hauna kuku wa maajabu, ila una maajabu ya kutisha.
Katikati ya msitu kuna eneo la mfano wa duara, hapo hapaoti miti na ndio panatajwa kwamba ni eneo la kushukia viumbe wa ajabu waitwao eliens ambao hutua eneo hilo kwa vyombo vyao visivyojulikana virukavyo angani.
Msitu umepata jina lake baada ya bwana Hoia-Baciu mfugaji mahiri wa kondoo kuingia msituni kulisha kondoo wake 200, yeye na kondoo wake walimezwa na msitu na hawakuwahi kupatikana tena.
Miongoni mwa mauzauza ambayo yamekuwa takiwapata watu wanaotembelea msitu huo ni pamoja na :-
° Kupotea. Wengi wa wanaoingia msituni humo hupotea na hawarudi kabisa.
° Kupatwa na magonjwa ya ajabu. Kuna ambao walibahatika kutoka kwenye msitu wa Hoia-Baciu lakini walirudu na magonjwa ya ajabu.
Wapo waliopata upele ambao haujawahi kuonekana duniani,wapo waliopatwa na majeraha ya Moto, na wapo waliopatwa na kipandauso
Pia wapo waliopatwa kichefuchefu kikali. Msitu huu pia huitwa Bermuda of Romania. Waromania Ni mahiri kwa uchawi, ushirikina na utumizi wa nguvu za giza