Msiyempenda kaja,Tambwe,Kamusoko na Ngoma kujiunga na kambi ya Yanga leo!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
KIUNGO Thabani Kamusoko na washambuliaji, Mzimbabwe mwenzake, Donald Ngoma na Mrundi Amissi Tambwe wanatarajiwa kuingia kambini leo usiku kuungana na wachezaji wenzao wa Yanga, kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba.

Nyasi bandia za Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam zinatarajiwa kutimbika kwa mchezo wa watani wa jadi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi kuanzia Saa 10:00 jioni.

Na wakati kikosi cha Yanga kikiwa njiani kurejea Dar es Salaam kutoka Shinyanga ambako Jumapili walishinda 4-0 katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Stand United, Kamusoko, Ngoma na Tambwe waliokuwa majeruhi wanatarajiwa kuungana na wenzao leo.

Watatu hao hawakusafiri na timu wiki iliyopita kwa mechi za Kanda ya Ziwa kutokana na kuwa majeruhi, lakini akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Msemaji wa Yanga, Dissmas Ten amesema kwamba wachezaji hao wataungana na wenzao leo.

“Ngoma, Kamusoko na Tambwe tayari wote wako fiti na wamekuwa wakifanya mazoezi kwa wiki sasa. Matarajio ni watajiunga na timu leo kwa mazoezi ya siku tatu zilizobaki kabla ya mechi na Simba,”amesema Ten.

Pamoja na kuwakosa wachezaji wake hao nyota watatu kwa muda mrefu, lakini imemudu kwenda sawa na mahasimu wao, Simba katika mbio za ubingwa.

Simba, Yanga pamoja na Mtibwa Sugar zote zinalingana kwa pointi hivi sasa, kila moja ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi saba na mshindi wa Jumamosi atatanua kwapa kileleni, wakati sare inaweza kuwashusha wote, iwapo Wakata Miwa wa Manungu watashinda dhidi ya Singida United Jumapili.
 
380d1d026ef61608ba67dc033107c5ab.jpg
7d8686053ca3c4d5fe27548871c95e3f.jpg
 
Iko sawa mnyama lazima achinjwe tu.
 
NGOJA MFUNGWE TENA MKONO! WATU HAWAJAFANYA MAZOEZI MIEZI MIWILI MNATAKA WAJE WACHEZE NA SIMBA
 
Kwani mara ya mwisho Yanga SC ilipofungwa na Simba SC na ile mechi ya Zanzibar pia hao Wachezaji ' tajwa ' hapo juu hawakuwepo? Miswahili bhana!
 
Kwanini umekasirika labda...?!

Unadhani Watu wote humu siyo wafuatiliaji wa mpira miguu huku ukiwa umesahau kwamba wengine humu tuna ' Vipaji ' vingi japo vingine tumevipunguza kutokana na ' majukumu ' mengine na pia ' umri ' nao kutuchukua. Nikusaidie tu ' technically ' Kocha wenu Lwandamina akisema awapange hao Wachezaji hiyo itakuwa ni ' suicidal ' kwa Yanga SC kwani bado wana tatizo la ' match fitness ' na hawatokuwa na ' tija ' yoyote kwenu sana sana mkiwachezesha hao mnaweza ' mkawatonesha ' majeraha yao halafu badala ya kuwapata ndani ya muda mfupi ujao sasa mkalazimika kuwakosa kwa muda mrefu na hata kupelekea kuharibu ' depth squad ' yenu na kuathiri perfomance yenu si tu katika VPL bali hata katika Makombe mengine kama Champions League na ASFC.

Lwandamina akiwa ' professional ' hatothubutu ' kuwapanga ' hao ' Wachezaji ' ila kwa ninavyowajua Viongozi wa mpira wa ' hovyo hovyo ' tulio nao hapa Tanzania na jinsi wasivyojiamini na waoga wa kupokea ' lawama ' kutoka kwa ' Mashabiki ' watamlazimisha Kocha awapange hao Wachezaji ' wagonjwa / majeruhi ' na ikibidi hata ' ganzi ' watawapiga ili tu wacheze na akikataa kuwapanga halafu Yanga SC ikafungwa basi haraka mno atafurumushwa / atafukuzwa katika Kibarua chake hicho.
 
Back
Top Bottom