Raia Mwema wakipata matangazo wayaweke tu kwenye gazeti lao, maana ni chanzo cha mapato. Ninachelea kusema kwamba wakati mwingine huwa najiuliza wanawezaje kuliendesha gazeti lile bila matangazo ya biashara. Kuna matangazo machache sana ambayo hayajitoshelezi kuendesha gazeti.
Kikubwa cha kuzingatia ni kuhakikisha makala zote zipo. Katika Raia Mwema linalolalamikiwa, sikuiona makala ya Joseph Mihangwa kitu ambacho kilinikwaza.
Mimi ni mmoja wapo niliyeudhika. kwenye ukurasa wa mbele wameandika nifungue ukurasa wa 39 ili kusoma makala inayomhusu mkuu wa takukuru nheshimiwa sana Dr Hosea na kauli zake tata juu ya EPA. Nikataka kufahamu amesema nini tena maana huyu kila wakati anatoa mpya! nimefungua na kukuta makala tofauti kabisa na hiyo iliyosemwa sikuiona ingawa pia iliyokuwepo ya Majid haikuwa mbaya.
Ni kweli biashara ya magazeti inataka matangazo lakini naamini katika hili hawakututendea
haki na naamini watatuomba radhi kwa vile 'Muungwana ni Vitendo'!
Wewe uliyandika ujumbe huu hauna maana hata blogu yako sitembelei -- kama kutangaza blogu ni kwa hoja kama hizi na lugha hizi basi wabongo tuna safari ndefu za mafanikio nina uhakika wewe utakuwa ni mhitimu wa mlimani
'Rais wangu' MMKijiji, hoja ipo! Jamaa hakusononeka peke yake, huko na sisi wa jikoni tulisononeka kuona gazeti limejaa orodha ya majina ya walimu. Hivi kwenye magazeti si huwa kuna supplements? Bora wangelituwekea kurasa zetu za kawaida halafu wakaweka supplement ya orodha ile.
.....
Mmesikia kuwa serikali imetoa notice kwa wizara kutopeleka matangazo yake kwa vyombo vya habari vya Mengi? Lengo ni kuua vyombo hivi na kumfanya Mengi aache kusimamia habari za ufisadi. Tanzania mtangazi mkuu ni Serikali - wanaJF tujue hilo.