Mkuu aka2030,
Awali ya yote karibu JF!Suala la kuporomoka kwa jengo haihusiana na usomi wa huyo mtu.Kwa kawaida engineer anatoa plan na kisha ujenzi unaendelezwa na mafundi.Sasa wakati mwingine mafundi hubania vitu kama saruji,nondo n.k katika ujenzi na hii hupelekea uhafifu wa jengo.Sasa sio kila mara engineer awepo pale kuhakikisha mifuko kadha ya saruji imekorogwa na kuchanganywa kwa kiwango husika.Sasa hili huwa tatizo na hatimaye hutokea nyufa na mwisho jengo kuporomoka.kwa hiyo wakati mwingine unatakiwa kufikiria kwa ufanisi na si kukurupuka.