Msongamano Court of Appeal utaisha vipi na lini?

Msongamano Court of Appeal utaisha vipi na lini?

SubiriJibu

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2009
Posts
1,805
Reaction score
1,876
Ndiyo mahakama inayoongoza kukatisha tamaa, siyo kwa kutotoa haki, hapana.

Court of Appeal ni mabingwa wa kutoa haki. Tabu yao ni kwamba ukiwa na kesi pale lazima uhesabu miaka miwili ndipo usikilizwe.

Matokeo yake baadhi ya majaji Mahakama Kuu (High Court) hulipua maamuzi yao wakitarajia wengi watakata tamaa kukata rufani Court of Appeal kwa ucheleweshaji.
 
Ni kweli kabisa, baadhi ya majaji wa mahakama kuu wanafanya maamuzi ya hovyo kwa makusudi na unaposema hoja kuwa kuna upendeleo anakwambia kata rufaa mahakama ya Rufaa akijua lazima ukate tamaa badala ya kukata rufaa.

Jaji mkuu awapangie vituo mikoani hawa majaji wa mahakama ya Rufaa wawe wanasikiliza kesi hukohuko vituoni mwao kama zilivyo mahakama za chini.
 
Back
Top Bottom