Msongamano wa makazi vijijini ni kipimo kikuu cha Jamii zenye akili: Waigbo wanaongoza kwa Waafrika

Msongamano wa makazi vijijini ni kipimo kikuu cha Jamii zenye akili: Waigbo wanaongoza kwa Waafrika

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187
Afrika ni Bara la pili kwa ukubwa duniani pamoja na kuwa na wakazi wengi huku likiwa linakaliwa na Waarabu, pamoja na Weusi (Blacks/Negro) wakitenganishwa na Jangwa la Sahara. Waafrika Weusi (Hamites, Negro, Bantu, Nilotes, San na Pygmy) wamekuwa wakiishi kwa muda mrefu katika Ukanda wa Tropiki (Hari), wenye joto jingi kwa mwaka mzima. Eneo hilo linalokaliwa na Blacks, lina mazingira magumu yaliyolitofautisha kabisa na Mabara menzake ya "Dunia ya Zamani (Old World - Asia & Europe)." Mazingira hayo magumu ni:
  • Uwepo wa joto jingi kwa mwaka mzima (kulipelekea energy depletion)
  • Uwepo wa mvua chache na zisizotabirika (unreliability) katika maeneo mengi.
  • Uwepo wa maeneo machache yenye rutuba ya kutosha.
  • Uwepo wa Ugonjwa hatari wa malale kwa mifugo (nagana) na binadamu (sleeping sickness).
  • Uwepo wa Ugonjwa hatari wa Malaria.
  • Kuchelewa kusambaa kwa teknolojia ya chuma.
Changamoto hizo kwa sasa, ni kama Nil but kabla ya kuja kwa Wakoloni in 1880s, changamoto hizo zilikuwa na nguvu kubwa sana katika mtawanyiko wa watu Afrika. Mfano: Bonde la Mto Congo ambalo ni kubwa kuliko Tanzania limekuwa likikaliwa na watu wachache kutokana na Ugonjwa wa Malale japokuwa ndilo eneo kubwa lenye mvua nyingi kwa mwaka mzima kuliko kote duniani (Old World).
Hata hivyo, kuna maeneo mengi madogo madogo barani Afrika, yenye sifa nyingi nzuri almost at par na maeneo bora ya Old World (Asia & Europe). Maeneo hayo yana msongamano mkubwa wa watu kutokana na kuzalisha chakula kwa wingi na kutokuwepo magonjwa mengi.
Maeneo ya vijijini yanayoongoza kwa msongamano mkubwa wa watu barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ni: Biafra (Waigbo) ikifuatiwa kwa karibu na Kilimanjaro (Wachaga). The Igbo are considered the brightest in Africa. Igbos Are The Most Brilliant Black Africa Race –US Report
Kwa Tanzania, msongamano mkubwa wa wakazi vijijini ukiacha Kilimanjaro uko: Arumeru (Wameru), Muleba (Wahaya), Rungwe (Wanyakyusa), Pemba (Wapemba), Ngara (Waangaza), Unguja (Watumbatu), Lushoto (Wasambaa), Ileje (Wandali), Morogoro (Waluguru), Buhigwe (Waha), Ukerewe (Wakerewe & Wakara), Newala (Wamakonde).
IMG_3738.jpg

Igboland

IMG_3595.jpg

Chaggaland

IMG_3593.jpg IMG_3596.jpg IMG_3582.jpg IMG_3581.jpg IMG_3565.jpg IMG_3549.jpg IMG_3527.jpg IMG_3521.jpg IMG_3472.jpg IMG_3712.jpg IMG_3475.jpg IMG_3555.jpg
 
Hapo naona kama idadi kubwa ya watu ndio inaweza kuwa the reason behind na kama sikosei IGBO ndio kabila lenye watu wengi sana Nigeria at around 32 million people
 
Hapo naona kama idadi kubwa ya watu ndio inaweza kuwa the reason behind na kama sikosei IGBO ndio kabila lenye watu wengi sana Nigeria at around 32 million people
No, siyo hivyo. Hii ni takwimu ya on per capita na siyo jumla ya watu. Kwa mfano: nchini Nigeria, Kabila la Igbo ni la tatu kwa watu likitanguliwa na Wahausa (Fulani) na Wayoruba.
 
Akha! mi nikajua utatoa sabubu za kwanini msongamano huo iwe kisabibishi cha kipimo cha uwezo wa akili!.
 
No, siyo hivyo. Hii ni takwimu ya on per capita na siyo jumla ya watu. Kwa mfano: nchini Nigeria, Kabila la Igbo ni la tatu kwa watu likitanguliwa na Wahausa (Fulani) na Wayoruba.

Kumbukumbu tatizo, anyway kwa idadi kama hiyo lazima wajae hata vijijini lakini pia hao jamaa ni kabila ambalo linaface segregation sana Nigeria so na point hii pia inaweza kuwa sahihi
 
Kumbukumbu tatizo, anyway kwa idadi kama hiyo lazima wajae hata vijijini lakini pia hao jamaa ni kabila ambalo linaface segregation sana Nigeria so na point hii pia inaweza kuwa sahihi
Nina uhakika na hili la watu coz nimelifuatilia tangu zamani kupitia Atlas mbalimbali za kabla ya 1970s. Na kwa taarifa yako, Waigbo huwa wanatajwa kuwa pia prominent kwenye ujasiliamali, Wachaga na Wakikuyu cha mtoto.
Jiji la Lagos liko mbali kwenye umbali wa km 500 kutoka Igboland tena kwenye Kabila kubwa kuliko wao na pinzani sana la Wayoruba but still wamekuwa tangu 1970s wakichangia 30% ya wakazi wake though kwa sasa, wastani umepungua kidogo.
Fikiria Tukuyu ama Bukoba jinsi zilivyokuwa mbali na uchagani na ziwe Makao Makuu ya Nchi halafu Wachagga ndio wawe asilimia 30% ya wakazi wa Bukoba ama Tukuyu.
 
Kumbukumbu tatizo, anyway kwa idadi kama hiyo lazima wajae hata vijijini lakini pia hao jamaa ni kabila ambalo linaface segregation sana Nigeria so na point hii pia inaweza kuwa sahihi
Ni kweli kuwa, wamekuwa wakibaguliwa na waliuliwa sana (Biafra War) baada ya Rais wa pili wa Nigeria (Muigbo) alipopinduliwa in 1960s lakini walikuwa tayari overpopulated ndugu.
Ni sawa sawa na eneo la uchagani ama mengine niliyoweka ya Tanzania - yote yalikuwa tayari highly populated huku Chagaland ikiwa overpopulated hata kabla ya kuja kwa Wakoloni in 1880s.
 
Back
Top Bottom