Lavan Island
JF-Expert Member
- Oct 24, 2015
- 2,377
- 2,048
Chukua tahadhari dhidi ya msongo wa mawazo, na wasaidie wengine jinsi ya kujiepusha na msongo wa mawazo na hofu zinazopita kiasi zinazotokana na mitazamo hasi ambayo hata hivyo mara nyingi haina uhalisia.
Msongo wa mawazo ni kipimo cha ukinzani wa akili na mwili dhidi ya mazingira yasiyo ya kawaida.
Ripoti mbalimbali za uchunguzi zinaonesha asilimia 60- 90 ya watu wanaougua, magojwa yao yanaambatana ama yanachangiwa na msongo wa mawazo.
Ni msongo wa mawazo ndio unaosababisha magonjwa kama vile ugojwa wa moyo (high blood pressure and diabetes), maumivu ya mgongo (back pain), maumivu ya kichwa (headaches), kukosa usingizi, matatizo ya ngozi, uchovu wa mwili wa mara kwa mara, kusahau na mengine kadhaa.
Mambo yanayosababisha msongo
Chunguzi nyingi zinaonesha kuwa hofu inayozalishwa maeneo ya kazi inachangia vifo zaidi 120,000 kwa mwaka duniani. Watu wengi wanaingia katika hofu ya kufikia malengo, ukubwa wa kazi, majungu kazini, manyanyaso kazini na mengineo. Katika kujaribu kushuhulikia haya watu wengi hutumia muda mwingi kufikiri kwa kina bila majibu na ndipo mawazo haya huwa endelevu kufikia kiwango cha kuathiri afya ya mwili.
Pamoja na changamoto za kazi, kwa ujumla zifuatazo zinaweza kuwa ni kichocheo kikubwa cha msongo wa mawazo:
vHofu ya kutopata kazi kwa muda mrefu
vChangamoto za kuongoza watumishi wenzi
vChangamoto za kimahusiano kazini
vKuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi
vKifo cha mwenzi wa maisha
vKuugua kwa muda mrefu bila matumaini ya tiba
vHistoria ya makosa kama ubakaji, madawa ya kulevya nk.
vMazingira magumu na yasiyovutia ya kazi
vNdoa ya kulazimishwa zaidi kwa wasichana
vTaraka
vKufukuzwa kazi
vChangamoto za kiuchumi
Chukua tahadhari dhidi ya msongo wa mawazo, na wasaidie wengine jinsi ya kujiepusha na msongo wa mawazo na hofu zinazopita kiasi zinazotokana na mitazamo hasi ambayo hata hivyo mara nyingi haina uhalisia. Na hata zile zinazoweza kutokea bado zaidi ya asilimia 70 ya hizo zinaufumbuzi.
Usichukulie mzaha – msongo unaua. Ni vema ukaacha mara moja na jenga utaratibu wa kupima msongo katika maisha yako. Msongo wa muda mrefu unaweza kusababisha ugonjwa na hatimaye kifo.
Usipojifunza namna ya kujipunguzia mawazo na hofu za kupindukia, msongo unaweza kuwa siraha kali ya kuangamiza maisha yako. Inawezekana kuwa sababu inayosababisha msongo kuwa siraha inayoua watu wengi ni kutokana na wengi pia kutokubali kuwa msongo ni siraha hatari ya kuangamiza maisha ya wengi.
Utafanyaje kujizuia dhidi ya madhara ya msongo?
Msongo ni jambo linaloweza kutupata kila siku katika maisha. Inahitaji uwezo binafsi wa kukabili msongo wa mawazo. Sina wasiwasi kuwa ikiwa utashindwa kujijengea uwezo wa kujizuia dhidi ya msongo basi utakuua.
Unazo njia mbili za kukabili msongo. Ni ama unatakiwa kukubali msukumo unaokuletea shinikizo na kufuata uelekeo wake ili kuleta mabadiliko chanya au fanya maboresho ya mazingira husika.
Wakati mwingine ni vema kukubali kushindwa kwa kuamua kuachana na ile nguvu ya msukumo kwa vile yapo mazingira ambayo kutofanya jambo ni bora kuliko kulifanya.
Kusoma vitabu vitakatifu hususani biblia ambayo ina methali na zaburi zinazotia moyo wenye hali ya kukata tama. Kwa hakika biblia inao ujumbe wa ajabu unaoburudisha moyo na kuleta matumaini makubwa.
Punguza muda wa upweke. Akili hujenga mfumo wa mawazo endelevu pale mtu anapokuwa pekee yake katika hali ya utulivu kuliko mtu anapokuwa katika majukumu na anaposhiriki kazi na mtu mwingine. Katika wakatia ambapo huna kazi ni vema ukajiwekea mazingira ya kusoma vitabu vinavyoweza kukujengea mfumo wa fikra chanya.
Acha kupuuzia mambo ya muhimu. Fahamu kwamba unaweza kupuuzia jambo la muhimu na kuamua kuliacha lakini ni vigumu kulisahau na hivyo kukupa wakati mgumu wa kukubali hasara ya kutolifanya.
Orodhesha mambo yako yaliyo muhimu unayotarajia kuyafikia au kufanya ili usisahau. Kwa sababu ya uwingi wa mambo unaweza kujikuta unasahau baadhi ya mambo muhimu na hivyo kujiweka katika msongo wa mawazo unaoepukika.
Kula vizuri. Lishe bora ya mwili na maji yakutosha inaupatia mwili balansi na kufanya kichwa kuwa chepesi. Lishe bora yaweza kuufanya mwili kukabili msukumo wa akili na mazingira kwa urahisi.
Kuwa na muda wa kubadilishana mawazo na familia. Angalau panga kula mlo mmoja wa pamoja na familia kwa siku. Itaweza kujenga upendo na kuondoa upweke miongoni mwa wanafamilia.
Usifiche matatizo moyoni. Tegua mabomu yote ya moyoni kwa kuwashirikisha mmoja wa mtu unayemuamini ili msaidiane kuleta suluhu. Eleza hali ya kutolizishwa na jambo, hii italeta amani moyoni mwako na akili itakuwa huru dhidi ya msongo.
Pangilia mambo yako. Watu wengi wasiofanikiwa siyo kwamba hawana mipango. Tatizo ni kwamba wanayo mipango mingi kiasi inawalemea katika utekelezaji. Kuwa na mipango mingi kutakuingiza tu katika mtego wa kushindwa kutekeleza na kubaki na msongo wa tafakari ya kushindwa. Ni vema kuchukua katika mikakati ya siku na ile ya muda mrefu vitu vile tu tunavyoweza kuvifikia kirasilimali na muda.
Kuwa na kiasi katika kutekeleza majukumu yako. Usipojizuia katika kazi ni rahisi kuvuka mipaka ya uwezo wa mwili na hivyo kujikuta unaufanya mwili na ubongo kuzoofika na hivyo kukosa uwezo wa kutekeleza hata mahitaji ya kawaida. Kwa hivyo ni vema kupanga muda wa kuanza na muda wa kumaliza kazi.
Wengi wetu tunayafahamu vizuri haya, lakini bado tunachelewa sana kuanza kuyachukulia hatu, tunaweza kuchelewa hadi yatakapoathiri kabisa maisha yetu. Tiba ni bora kuliko kinga na ni vema kila wakati kuanza kutekeleza kile unalichokigundua kuliko kusubiri.